Pia yumo Ishmael MBISE. Huyu kwa sasa ni Profesa wa Literature, Chuo Kikuu Tumaini Makumira. Aliandika: Blood on Our Land. Waandishi wa Kazi za Fasihi wako WENGI tu. Pamoja na Shaaban Robert, wapo pia: Kezilahabi, Semzaba, Aldni Mutembei, Mulokozi, Angoro Anduru, Kaigarula, Penina Muhando-Mlama, Ebrahim Hussein, Richard Mabala, Profesa Mbogo, Julius Nyerere, Gabriel Ruhumbika, Amandina Lihamba, Balisidya, Ndulute, nk. Wengi wa hawa waliandika kazi zao za Fasihi kwa lugha ya Kiswahili.
Ieleweke pia kuwa Africa Writers' Series, ni kampuni la uchapishaji wa kazi za Fasihi za Kiafrika (zilizoandikwa na Waafrika) kuhusu Afrika. Lugha ya uchapishaji ni Kiingereza. Kwa maana hii, kukosa kuchapisha kazi ya Fasihi katika AWS, haimaanishi Watanzania Hawajabobea katika kazi za Fasihi. Kwa waliosoma Fasihi shule za sekondari na vyuo, wamesoma kazi nyingi tu za fasihi zilizotayarishwa na Watanzania.