Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

Hoja:
Afrika ina nchi zaidi ya 50, mbona umezitaja nchi 3 tatu, iweje uishangae Tanzania wakati hata nchi nyingine hazina African writers mfano Malawi, Angola, Chad, Afrika ya Kati, Somalia na Msumbiji.

Nahisi exposure kutokana na elimu ya mkoloni ndio ilisaidia baadhi ya nchi kuchangamka mapema. Kwa mfano, Wanaijeria walianza kupata elimu nzuri na exposure kipindi cha mkoloni nahisi kuliko nchi nyingine ya Kiafrika. Chinua Achebe aliandika novel ya Things Fall Apart mwaka 1957 wakati Tanzania tupo na mapambano ya TANU.

Uganda ndiko kulikuwa na Makelele University, hivyo exposure ilikuwepo.

Kenya setlers walikuwepo, hivyo exposure ilikuwepo.

Afrika Kusini licha ya kuishi Wazungu kwa miaka zaidi ya 600 lakini kulikuwa na sera ya ubaguzi wa rangi hivyo ilikuwa ngumu kwa Waafrika kupewa elimu nzuri.

French Colonies wao walikuwa bize kwenda Ufaransa na kucheza mpira kutokana na sera ya Assimilation policy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…