Wanaochukulia maisha simple tu ni wapuuzi na hawajali afya zao na za wale wanaowazunguka. Ni lini serikali imetangaza corona imeisha watu waache kuchukua tahadhali?
Yaani wewe kila siku unaambiwa uchukue tahadhari unapuuza eti kwa kuwa hautangaziwi takwimu mpya. Watu kama hawa ni wa kuwapima vyote, corona na akili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Iko wazi mkuu, muamko umepungua sana kwenye jamii. Ile kunawa mikono na kuvaa barakoa imepungua. Kama wewe ni mfatiliaji na "mzururaji" mzuri utaelewa kile nachomaanisha.
Mimi kuchukua tahadhari zote wakati wengine wanachukulia simple tu bado haitoshi kunihakikishia usalama wangu. Mwanzoni kwenye vituo vya bodea boda ,bajaji na kwenye maduka kulikuwa na ndoo za maji na sabuni, watu walikuwa hawapati huduma bila kunawa mikono. Ila kwa sasa zile ndoo nyingi ukikagua utakuta hazina maji, sabuni hakuna, pia watu hawanawi mikono tena kwea sana kama sharia ili ndio wapate huduma.
Tuliweza kudhibiti huu ugonjwa na kupunguza madhara kwa kuwa mwanzoni tulichukua tahadhari kwa hali ya juu. Na hilo limeleta matokeo chanya ndio maana hadi sasa hali iko vizuri. Ila kwa sasa kuna kujisahau kidogo na kulega lega, kitu ambacho sio kizuri maana ugonjwa bado upo. Msisitizo na uelemishaji uendelee kwa kiwango kile kile kama awali.