Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Na kwa saivi maeneo yalivyo jaa hakuna sehemu ya kusema watatenga iwe hivyo labda mpaka wahamishe watu, kitu ambacho sidhani kama itakua rahisi kutokea
 
Kama umetoka nyumbani unaenda kukutana na Mgeni wako mjini

Unabidi uwe na hela ya kinywaji tofauti na hapo mtaongea mmesimama hadi mnaagana.
Hakika, Inasikitisha sana.
 
Kwa viongozi waroho wanaouza hadi open space wajenge magorofa , dar , mbeya , mwanza, Arusha kulitakiwa kuwepo na bustani za watu kupumzika ambazo zina mandhari nzuri yenye kueleweka na sio iwe moja mfano Dar kigamboni , Tabatha, mbezi, kote kila watu walipaswa wawe na bustani zao na kwa mkoa wenye joto kama Dar kunakua na bwawa la kuogelea kabisa wananchi wawe wanaoingia bure wanaondoa misongo yao ya mawaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…