Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Kwasababu ya mabadiliko ya tabia nchi
 
Faida ya sehemu ya kupumzikia ni kwanza kuondokana na msongo wa mawazo yaani stress free zone, lakini pia watu kukutana kupanga biashara zao , wengine wachumba hukutana maeneo kama hayo, lakini pia kupumzika kwa watu wote hasa siku za juma
 
Kimsingi hio mnazi mmoja kuanzia Morogoro road hadi nkuruma road ilipaswa kuwa open space...garden nk wameipunguza...basi eneo lililobaki waliboreshe...

Posta kule kuna Botanical garden ile imeachwa tu...ile nayo ilipaswa kuwa open garden ya watu kupumzika
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Ukiweka akija mwekezaji na hela zake anajenga hata sheli {kituo cha kujazia mafuta}
Nchi yetu tunaijua wenyewe
 
Watu watakueleza cocobeach wakati ilitakiwa public beaches ziwepo nyingi zikisimamiwa na halmashauri mbalimbali
 
Yani jiji la dar liko ovyo mno, kuna hao waliouza maeneo ya wazi na pia kuna wakuitwa machinga ni janga huko masokoni tu wamejazana wao hadi sehemu za wateja kusimama kununua bidhaa wapo wao, hizo opening space watakuja na vitoroli vyao wajazane, ila jiji hili tunaishi kwa mateso sana
 
Yani jiji la dar liko ovyo mno, kuna hao waliouza maeneo ya wazi na pia kuna wakuitwa machinga ni janga huko masokoni tu wamejazana wao hadi sehemu za wateja kusimama kununua bidhaa wapo wao, ila jiji hili tunaishi kwa mateso sana
Machinga ndio wapiga Kura wenyewe, ndio maana Wal-Mart walikua wanafanya tafiti za kujenga malls kwenye miji mikubwa Tanzania wakaondoka na jibu kua maduka ya manunuzi kwa Tanzania hayawezi kufanya vizuri maana kila nyumba ina kibanda, yaani matumizi ya maeneo kibiashara na makazi haieleweki ndio maana utakuta kwenye makazi kuna gest za showtime, bar, danguro, kabisa, msikiti , yaani balaa tupu
 
Noise pollution kwa Tanzania tunashangaza pita masokoni huko mbagala, mbeya, mwanza, Arusha, na maeneo mengi kila duka na spika na vipaza sauti maeneo hayana utulivu wastaarabu wakifika wanaona kabisa hii jamii haijaelimika kiufupi ni washamba
 
Machinga ndio wapiga Kura wenyewe, ndio maana Wal-Mart walikua wanafanya tafiti za kujenga malls kwenye miji mikubwa Tanzania wakaondoka na jibu kua maduka ya manunuzi kwa Tanzania hayawezi kufanya vizuri maana kila nyumba ina kibanda, yaani matumizi ya maeneo kibiashara na makazi haieleweki ndio maana utakuta kwenye makazi kuna gest za showtime, bar, danguro, kabisa, msikiti , yaani balaa tupu
Mambo ni vanga vanga, mtu akiamua anafungua kanisa nyumbani kwake, hapo hapo kuna vigodoro na kibanda umiza mara genge ukivuka nyumba ya pili kuna guest bubu ni mvurugiko tu
 
Yani jiji la dar liko ovyo mno, kuna hao waliouza maeneo ya wazi na pia kuna wakuitwa machinga ni janga huko masokoni tu wamejazana wao hadi sehemu za wateja kusimama kununua bidhaa wapo wao, hizo opening space watakuja na vitoroli vyao wajazane, ila jiji hili tunaishi kwa mateso sana
hama!
 
Back
Top Bottom