Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Imeangaliana na jengo la ofisi ya ccm mkoa,pia jirani na ofisi ya wilaya ya nyamagana ya zamani. Karibu na daraja la mirongo
Kemondo stand ipo wapi/ sehemu gani hapa Mwanza mjini?. Kuna wakati huwa natamani kukaa mjini nipoteze masaa lkn naishia kutembea tembea tu.
 
Ikiwa mwenge pala masheikh ubwabwa wameuza msikiti ili yajengwe maduka.
Na coco beach wanajenga msikiti hii inakueleza kwamba hatuns akili kabisa.

Ubepari uchwara tunaoufuata unatufanya mpaka road.reserve zinauzwa yanajengwa maduka. Car wash. Mihogo point shop na chips shops.

Aliyetuloga alikufa na mchonga
 
Huwezi elewa uzi wa mleta uzi mpk utembee kwenye nchi za watu wengine. Tuna viongozi wajinga sana kupata tokea duniani. Na kibaya ni kuwa watanzania wengi hawana Exposure duniani huko. Mtu anasoma la kwanza mpk form 6 kijijini kwao huko, chuo ndio anakuja mjini UDSM ghafla kamaliza chuo ndie afisa ardhi/ mipango wa mji, unategemea atapanga mji wa kisasa huyo?
 
Mwanza nadhani ipo japo nina mda sijaenda pale Kemondo kwani pameuzwa?

Dar napo kituo cha posta ya zamani hapo NBC kama sijakosea japo ni padogo na pale mwembe yanga

Dodoma ipo Nyerere square pako sawa kibongo bongo

Morogoro sijui kama wanayo.


Iringa juzi nimepita sijapaona
 
Mi ninavyojua zipo.

Magomeni, Sinza Darajani
 
Znz zipo za kutosha
Kinondoni,mwananyamala zilikuwepo nyingi ccm wamezigawa nyingi na kuwapa watu wafanye biashara magereji nk...hawa jamaa maeneo mengi ya wazi walijimilijisha kama mali ya chama
Ile biafra ione leo ilivyokuwa....
Hata ile eneo cha chuo kikuu huria ni maeneo ya wazi kushuka mpaka chini yote yale maeneo y wazi

Ova
 
Mbona ipo moja nzuri sana maeneo ya Chanika.
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
o m
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?

Sisi mjini maana yake ni m'mbanano wa majengo na manyumba
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Ile ya posta dsm ni nini,ile ya Dodoma Nyerere square ni nini?
 
Ni kwa sababu tuna planners wabovu. Yaani wanataka kila eneo liwe kiwanja cha kujenga ili wauze plot nyingi. Kuna maeneo makubwa unakuta yamepimwa lakini hata kiwanja cha kuchezea watoto hakuna, zahanati hakuna na wakijitahidi sana ni kaeneo kadogo ka soko.
 
Back
Top Bottom