Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Ccm wamekata viwanja kwenye hizo open spaces
 
Boss coco beach yenyewe ile baada ya miaka kumi itakuwa huwezi kuiona bahar kama huna hela ya bia yan hawa wawekezaji uchwara wanasumbua sana kwenye maeneo ya wazi mtu kila sehemu ukitaka kusimama unaona bango marufuku kusimama hapa open space zinajengwa apartments au kugeuzwa yard za vibopa
 
Kuna open garden inaitwa forodhani pale Tanga. Mchana ni sehemu ya watu kupumzka, ucku ni danguro, watu wanakulana kwny hvyo vikochi vya zege, unafika asubuhi mida ya saa 4 unapoa zako unakutana na likondom hapo. Dahh tokea nilivokutana na hii hali sikuwa natimba tena ile garden ya forodhan.
ule uchafu unatia sana kinyaa

mkuu pole sana
 
Pale Magomeni Garden kidogo kidogo watu wamevamia mpaka kumebaki hovyo kabisa, pale Mnazi Mmoja hata kuvutia hakuvitii na hakutunzwi.
 
Tatizo ni kwamba hakuna mipango miji na wanaouza viwanja sio serikali ni watu binafsi hapo ndiko tatizo linakoanzia
 
Sema wadada tutajaa sana...
Then mtuambie kwamba tunaji-sale..
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Watu wa ardhi na Mipango miji ndio wa kulaumiwa. Wanachowaza ni rushwa tu , kupendezesha miji na kutengeneza recreational sites sio kipa umbele.
 
Magomeni tu hapo zilikuwepo 3,kubwa ilikuwepo pale kanisani kwenye opposite na hospitali ya magomeni,nyingine ilikuwepo mikumi mtaa wa msanga,mpaka lile eneo linaitwa garden ila kushauzwa na kuna mijengo na parking za hotel,nyingine magomeni kondoa,posta front ya nbc bank ilikuwepo na mabenchi yake ila kwa sasa yamebaki maua tu na watu awaruhusiwi hata kusimama kwa dk 2,maeneo kama ya gymkhan ni mazuri ya kupumzika pia ila utakuta wengi wao ni wadosi ndio wamechill unaweza hata kubaguliwa ukifanya masihara
 
Binafsi nikiangalia baada ya kituo cha mabus mwenge kufunguliwa,kile kituo cha simu 2000 isingewekwa yard ya brt,pale ingejengwa park kubwa,kikubwa kuzuia wamachinga wasijazane miamvuli yao,dar ina sehemu nyingi nzuri zinaharibiwa na wamachinga,kama mbezi mwisho serikali inashindwa kweli kuwatafutia eneo wamachinga wakawaondoa mle barabarani na miamvuli yao inafanya eneo lionekane chafu
 
Posta pale zipo...sema kwa bongo huwez kupumzika maana inakua sehem ya madalali kuuza bidhaa zao
Watafanya kaz saa ngap sasa bongo mtu atatoka asubh na maji ya kuzungia wee atamaliza sku nzma kla sku kwa kukaa free mwsho wa sku atakuwa anawaza atapataje connection ya kwenda kwa P dydd awe bilionea au kbaka mm naona syo utamaduni wetu ss Waafrka tunatakiwa tupge kaz pumzka kwako
 
Morogoro municipal ivunjwe waweke open spaces pale km zamani. Kwa sasa hakuna sehemu za kukaa labda dukani kwa mtu.
 
Changamoto nyingine kubwa ya sisi Watz IPO sehemu moja.

Sehemu ya kupumzikia inageuzwa guest house

Mfano ukienda mwembe yanga ni aibu Sana kiukweli.
Wacha watu wadinya e bwana...perfectly natural thing to do
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Kwa viongozi waroho wanaouza hadi open space wajenge magorofa , dar , mbeya , mwanza, Arusha kulitakiwa kuwepo na bustani za watu kupumzika ambazo zina mandhari nzuri yenye kueleweka na sio iwe moja mfano Dar kigamboni , Tabatha, mbezi, kote kila watu walipaswa wawe na bustani zao na kwa mkoa wenye joto kama Dar kunakua na bwawa la kuogelea kabisa wananchi wawe wanaoingia bure wanaondoa misongo yao ya mawaza
Tatizo hili la kukosekana kwa Open Spaces kwa Tanzania limesababishwa na janga la Kifo cha Mipango-miji katika nchi. Ardhi kubwa sana katika nchi hii haipo katika Mipango-miji na Wala haijapimwa. Miji mingi Sana ipo shaghala-baghala, ni Squatters.

Aidha, hata kwenye baadhi ya miji ambayo imepimwa na ambako kuna Mipango-miji, maeneo ya wazi au Open spaces nyingi Sana zimetwaliwa na baadhi ya Watu/Viongozi au Watendaji wa Serikali au Viongozi wa Chama tawala cha CCM, maeneo hayo ya wazi yamegeuzwa kuwa Viwanja vya Kujenga Majengo binafsi ya Makazi au Biashara.

Vile vile, CCM nayo imepora kwa wingi Sana maeneo hayo na kisha kujenga Ofisi zake au kujenga Majengo ya Maduka "frames" za kupangisha Watu na wao wamekuwa wakikusanya Kodi kutoka kwa Wapangaji. Mathalani, maeneo karibia yote ambayo yanaitwa kuwa ni "Viwanja vya Sabasaba" ambayo yametakapaa hapa nchini yalikuwa ni maeneo ya Open Spaces kwa ajili ya matumizi ya umma. Hata hivi viwanja vya Mpira ambavyo vimeporwa na CCM na kuvifanya kuwa Mali yake binafsi vyote kabisa vimejengwa kwenye Open Spaces. Mfano wa viwanja hivyo ni CCM Kirumba-Mwanza, Uwanja wa Jamhuri wa Morogoro na Dodoma, n.k.
 
Meanza ipo moja pale kemondo stand japo sidhani kama privacy ya mtu inazingatiwa au ndo kukurupukiana tu kulazimisha stories
Kemondo stand ipo wapi/ sehemu gani hapa Mwanza mjini?. Kuna wakati huwa natamani kukaa mjini nipoteze masaa lkn naishia kutembea tembea tu.
 
Watu wenye wajibu huo wako ofisin ni kunywa kahawa kucheka Cheka jion wanarudi majumbani kwao
 
Back
Top Bottom