Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Kwanini Tanzania hatuweki open spaces za watu kupumzika katikati ya miji?

Mtu unahitaji kufanya mazungumzo na mwenzako, unalazimika kwenda bar coz hakuna sehemu ya wazi mtakutana muongee. Recreation centers ni muhimu sana, watawala hata hawajui hilo.
 
Moshi palikuwa na Uhuru park sijui watakuwa wameshagawana viwanja wale jamaa zangu wapenda ardhi au kama ipo sijui ina hali gani?
 
Mh. Makonda enzi za ukuu wa mkoa wa Dsm alituahidi atazitengeneza za kumwaga, ataweka taa mji mzima na Kariakoo itakua soko la masaa 24, hadi anaondoka mitamboni hakuna kilichotokea,

Ile ya Posta after mazoezi nilikua mdau wa kukaa pale kutuliza akili na ilinipatia wachumba sana 🤭
 
TZ nchi ya kipumbavu sana. Watu wa mipango miji sijui wanasomea ujinga huko shuleni hakuna sehemu hata moja imepangika hii nchi.

Coco beach ilikua a public beach leo pamejenga hadi majini kabisa.

Mbeya lilikuwepo eneo la wazi karibu na uwanja wa sokoine leo limekua soko.

New York kuna central park. Chicago kuna Lake shore drive haya ni maeneo ya wazi katikati kabisa ya miji na hamna mtu anagusa ila bongo wakiona uwazi tu ni kuweka frame, club, kanisa au msikiti. Nchi ya kipumbavu sana hii.
Hawa watawala wetu huwa hawajifunzi wakienda huko nje na kutamani kupapendezesha kwao wanapotokea kuwe kama huko kwa waliostaarabika??
 
Ccm wameZinywa maeneo mengi ya wazi

Ova
 
Maisha ya bongo sio lele mama hakuna muda wa kupumzika
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?
Uchoyo, ubinafsi na siasa vimetawala yaani umaskini wa kufikiri.
 
Mfano Tanga Kuna mahali nilipita, karibu na maktaba ya mkoa Kwa pembeni kitu kama forodhani hivi wanaita kama sijakosea, eneo lile limetengenezwa vizuri sanaaa, siku za wikiendi unakwenda unatulia na hata soga unaweza piga na mwenzako, bahari unaangalia Kwa chini kulee...zikipatikana sehemu kama hizo tena ziwe kubwa kiasi ni vizuri kabisa.
 
Mwanza ipo moja pale kemondo stand japo sidhani kama privacy ya mtu inazingatiwa au ndo kukurupukiana tu kulazimisha stories
 
Zilikuwepo sema zote wameuza maana viongozi wetu vitu vizuri hawataki kuviona
 
Hawa watawala wetu huwa hawajifunzi wakienda huko nje na kutamani kupapendezesha kwao wanapotokea kuwe kama huko kwa waliostaarabika??

Hao ndo empty set kabisa. Sio kwenda tu nje wengi wamesoma nje na kufanya kazi kabisa ila wakirudi bongo akili zinaruka.

Majengo, barabara, shule, hospital, mipango miji ya enzi za mkoloni ni bora kuliko miundombinu inayojengwa na wamatumbi leo. Nchi ya kipumbavu sana hii.

Magu alikataa Coco isijengwe kafariki tu leo coco kuna kila aina ya takataka.
 
Kwanini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza hakuna open spaces katikati ya miji kama Nairobi wakati Tanzania tuna ardhi kubwa kuliko Kenya?

Upumzike kwa raha gan... wakiweka kesho utakuta mtu kapanga pipi /viatu au meza ameshageuza kizimba cha biashara mwishoe utazungushwa ukuta na bango la kupiga marufuku kuingia

We huoni vituo vya basi watu wanavyopanga bidhaa

Tuko nyuma mda Tutapumzika mbinguni
 
Open spaces ziwekwe na mgambo wa majiji wafanye kazi yao.
 
Ni nzuri sana nyakati za usiku hizo.... stress kede waenda kupigwa kibaridi hapo
 
Back
Top Bottom