Tanzania ni moja ya nchi zilizopo mashariki mwa bara la Africa. Na ndani yake huishi Watanzania na asilimia ndogo ya watu kutoka nchi zingine duniani. Tanzania sasa angalau haipo katika nchi maskini duniani, sasa ni nchi ya uchumi wa kati.
Nchi hii imebarikiwa sana, ina rasilimali nyingi ambazo kama zingetumika ipasavyo basi watanzania wangekuwa tajiri duniani kote.
Kutokutumia vizuri rasirimali zilizopo kumesababisha watanzania wengi kuwa na kipato cha chini ilihali nchi yetu imesheheni rasilimali.
Rasilimali hizo ni kama vile ardhi nzuri yenye rutuba, madini, vyanzo mbalimbali vya maji ikiwemo bahari ya Hindi ambayo ni nyenzo muhimu kwa usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi na kuja ndani, misitu, mbuga za wanyama wa aina mbalimbali pamoja na rasilimali watu.
Hapa chini ni picha ambazo zilichukuliwa kutoka mbuga ya mikumi mwezi April 2022 nikiwa katika utalii wa ndani na kujionea rasilimali za Tanzania.
Mbali na hayo fikiria ile Ruby gafi ya uzito wa kilogram 2.8 iliyoingia katika mnada huko Dubai na kuishangaza dunia kwa ukubwa wake na kupigwa mnada wa $120
Fikiria pia kuhusu mawe makubwa ya Tanzanite yaliyochibwa huko Mererani hivi karibuni. Hakika Tanzania ni tajiri.
Zifuatazo ni sababu ambazo zinaifanya Tanzania kuwa na uchumi usio imara licha ya kuwa na rasilimali nyingi.
Ukosefu wa elimu maalumu. Elimu itolewayo mashuleni hasa shule za msingi ni elimu jumuishi ambayo haitoi kipaumbele kwa uwezo binafsi wa mtoto tangu akiwa mdogo ili kumfanya abobee katika kile anachokipenda, na kwa hali hii tumebaki na elimu kinadharia tu, lakini vipaji vingi vinadidimizwa ambavyo vingekuwa tunu kubwa kwa kusimamia na kutumia rasilimali za Taifa katika nyanja mbalimbali na kuleta maendeleo makubwa ya taifa kiuchumi.
Lakini pia tabia ya wazazi na walezi kuwachagulia vijana wao tasnia za kusoma kunapoteza ufanisi wa kazi. Kwa mfano, rafiki yangu mmoja alikuwa na ndoto ya kuwa mvuvi, alihitaji kwenda kusomea uvuvi, sasa akawambia wazazi, wazazi wake walikataa na kumlazimisha kwenda kusoma udaktari kwa kuwa huko atapata ajira kirahisi, na kweli akasoma udaktari na sasa ana digrii, kwa hiyo amekuwa daktari kwa sababu ya wazazi lakini moyoni mwake yeye ni mvuvi.
Wahitimu kushindwa kuweka elimu waliyoipata katika vitendo. Wahitimu wengi wameshindwa kutumia rasilimali zilizopo kujitengenezea kipato kwa kuwa ile elimu ya nadharia wameshindwa kuiweka katika matendo kama vile kulima,kuuza na kununua Mari ghafi na bidhaa za kitanzania, kuchonga, kufundisha watu wngine kuhusu ujuzi Fulani n.k na ndio maana hata kujiajiri inakuwa ngumu.
Sababu nyingine ni kupungua kwa nguvu kazi katika sekta mbalimbali za jamii kama vile afya, elimu, kilimo, uchukuzi na ujenzi. Hapa watenda kazi waliopo katika hizi nyanja hawatoshi ukilinganisha na wanaohitaji huduma ingawa huku mtaani tunao wataalamu wengi kutoka vyuo vikuu, kwa mfano mnamo April 2022 serikali ilitoa kibali cha ajira za walimu 9,800 lakini walioomba hizo ajira ni walimu 123,390 tunaweza kuona kuwa hakuna uwiano mzuri kati ya hizo nafasi na wahitaji , lakini pia baadhi ya hao watumishi waliopo wamezeeka na ufanisi wa kazi umepungua.
pia Tabia ya vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kubweteka vijiweni na kupiga sIkiwezekanamiza sana uchumi wao ukizingatia muda na nguvu wanazopoteza katika hili swala.
Pia mitazamo na maono kinzani ya viongozi wa umma ni sababu ya uchumi usio imara. Kiongozi huyu Leo anasema tujenge hapa uwanja wa ndege, tunaanza kujenga, akitoka madarakani akija mwingine kesho anasema hapana tusijenge hapa tujenge kulee, hii husababisha pesa za miradi ya serikali ambazo baadhi ni kodi za raia kutumiwa ndivyo sivyo na kuchelewesha maendeleo yetu
Mapendekezo ya nini kifanyike kujenga uchumi imara
Mtaala wa elimu uzingatie kuwaandaa wajuzi mahiri kwa kuzingatia vipaji vya watoto kwani Siku zote mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.Tuache kujikita sana na elimu jumuishi na kujikita katika elimu maalum. Tunapoteza wakulima, rubani, wachoraji, wavuvi selemala, na makandarasi wengi katika ngazi za chini za elimu.
Wazazi na walezi, wapeni watoto uhuru wa kusomea fani wanazozipenda wao kwani hii itawawezesha kupenda kazi zao na kuzifanya kwa weledi zaidi huku wakiwa ni wenye furaha.
Taasisi za elimu za umma na binafsi wapeni vijana mbinu za maisha na namna ya kuibadili elimu waliyoipata kuwa kipato, natamani kuwepo na utaratibu wa mafunzo kwa vitendo kwa kipindi cha mwaka mzima kabla mhitimu wa chuo kikuu kutunukiwa shahada.
Kuwepo na sheria inayozuia vijana kukaa vijiweni Masaa ya kazi na Siku za kazi, ili iwawajibishe kwa faida yao na taifa kwa ujumla. Ikiwezekana yaandaliwe mashamba ya serikali atakaye kutwa amezuba zubaa mtaani apelekwe huko akalime, ili tuepuke changamoto za uhaba wa alizeti , ngano, pamba n.k.
Napendekeza kuwepo na utaratibu maalumu unaomuongoza kila kiongozi anaeingia madarakani kuhusu miradi na rasilimali za nchi. Kuwepo na sauti moja kwa kuwa wanajenga nyumba moja. Hii itaondoa mitazamo kinzani baina ya viongozi na ubinafsi hautakuwepo tena.
Umri wa kustaafu uangaliwe upya, natamani ushushwe mpaka miaka 50. Ili zipatikane nafasi za kazi kwa ajili ya hawa vijana wenye 30+ bila ajira.
Mungu endelea kuibariki Tanzania na watu wake.
Nakaribisha maoni na maswali.Naomba kura yako pia.

Upvote
2