Kwanini Tanzania Masikini? Masaa mawili tunamsubiri Naibu Waziri Mkuu Biteko apite

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Tangu nizaliwe, nilikuwa nasikia Viongozi wanaleta Foleni.

Nipo huku Shinyanga, tumesimamishwa masaa mawili sasa tukisubiri Dotto Biteko apite.

Ng'ombe wangu watafika mnadani saa ngapi? Hasara tayari. Mikopo ya Vikoba itanitoa roho.

Viongizi wa Tanzania jitafakarini

 
Salaam Wakuu,

Tangu nizaliwe, nilikuwa nasikia Viongozi wanaleta Foleni.

Nipo huku Shinyanga, tumesimamishwa masaa mawili sasa tukisubiri Dotto Biteko apite.

Ng'ombe wangu watafika mnadani saa ngapi?

Viongizi wa Tanzania jitafakarini
Umekosea sana uliposema ''viongozi wa Tanzania jitafakarini''. Wajitafakari nini wakati hawana cha kutafakari? Wananchi ndiyo wanaotakiwa kujitafakari jinsi walivyogeuzwa kama manyumbu ya kule Manyara mbugani. Ingekuwa vizuri sana kama wangeongeza masaa ya kusubiri na kusema siku kiongozi anapita eneo fulani, hakuna ruhusa raia kupita hilo eneo siku nzima.
 
Upo sahihi. Eti mteule wa Samia kavimba kichwa anatutesa Wabara.

Tunaomba mtusaidie turuhusiwe kutoka hapa Bukombe. Tupo chini ya miguu yenu Waheshimiwa.

Watoto wanateseka Maporini
 
Hakuna namna. Wenyewe "viongozi" ndiyo wanapenda iwe hivyo Lakini mwisho wa siku zigo wanaangushiwa Polisi.
 
Ishu sio viongozi bali ni wasimamizi wa usalama barabarani ambao timing ya kuzuia magari huwa wanaikosea
Wote tu, toka viongozi, wasimamizi wa barabarani na wananchi..!! Waziri mkuu alishawahi sema juu ya jambo kama hili kwenye msafara wake, ingawa inakuwaga unafiki tu maana baada ya hapo yanaendelea yaleyale yaliyoonekana kukemewa..!!
 
Zamani tulikuwaga tunapishana nao, kupuuza huku sokoine akafa, wazifi mkuu wa sweden alalf palme alikuwa anaenda sokoni kama raia wa kawaida akapigwa risasi alafa, ndo maana tumestuka, usalama kwanza
 
Zamani tulikuwaga tunapishana nao, kupuuza huku sokoine akafa, wazifi mkuu wa sweden alalf palme alikuwa anaenda sokoni kama raia wa kawaida akapigwa risasi alafa, ndo maana tumestuka, usalama kwanza
Nakubaliana na wewe kuhusu usalama wa viongozi lakini a point of correction.Waziri Mkuu wa zamani wa Sweden Olof Palme hakupigwa risasi akienda sokoni bali alikuwa akitoka kwenye jumba la kuonyesha filamu akiwa na mkewe Lisbeth Palme.
 
Tanzania itakuwa nchi maridadi pindi tu watu wake watakapoamua kuacha UNAFIKI.
 
Asanteni Wakuu, Biteko kapaki Pembeni ili Magari yalosimama zaidi ya masaa mawili yapite. RTO wq Shinyanga anayakiwa ajiuzulu. Hii ni international road. Kusimamisha magari masaa mawili na dakika 45 si sawa. Mmalori mengine yanebeba sumu na mengine ya kulipuka.
Anyway, asante kwa msaada wenu Wakuu. Tumeruhusiwa
 
Naunga mkono hoja
 
Hapo ndipo tofauti kati ya mheshimiwa na mnyonge ilipo. Wakati fulani enzi hizo, watu wote walikuwa ndugu moja, kiongozi aliitwa ndugu kama wananchi wengine wa kawaida.

Majira yamebadilika, nyakati zimebadilika, hivi sasa uchawa ndiyo habari mijini na vijijini. Uchawa, kujionyesha, na kujipendekeza ndiyo siri ya kukumbukwa na kupewa vyeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…