Kwanini Tanzania tumeng'ang'ania uchumi wa frame za maduka? Mbona hata ufugaji unalipa?

Kwanini Tanzania tumeng'ang'ania uchumi wa frame za maduka? Mbona hata ufugaji unalipa?

Hizo bidhaa za shambani kwako kama mayai, nyama na maziwa zinanunuliwa kwa mkupuo kwenda kwa mlaji wa mwisho?
Lazima kuwe na supplier hapo katikati na huyo supplier lazima awe na eneo/nyumba ya biashara, ndo frame unazozilalamikia. Hata ukisema tujenge viwanda bado frame zitabaki na umuhimu wake tu bidhaa zinazozalishwa huko viwandani zinasambazwa na hawahawa wafanyabiashara wa kwenye fremu.
Kuna uzi kama huu nilijibu kama hivi. Mtu anabeza retailers anasema watu wajikite kwenye uzalishaji. Sasa genius huyo anaewaona retailers hawana maono haoni kuwa akishazalisha atahitaji retailers kuuza bidhaa zake!
 
biashara ya viumbe vyenye roho ni risk sana. Nishashuhudia mtu akizika kuku zaidi ya 3000 kwa wakati mmoja .
Pamoja na hivo,hata kwenye makampuni Kuna kufilisika, kuachishwa kazi,mishahara kidogo nk.
Kwa upande wa kilimo, Kuna ukame, wingi wa mvua, na swala la soko pia.
Kwa hiyo kila pahala Kuna changamoto zake
 
Real estate ni biashara nzuri ambayo ina costs chache (maintenance). Thamani yake inapanda kila mara japo not 100% guaranteed kuna factors zinazoweza kufanya usipate faida.

Lakini uki compare na biashara nyingine kujenga nyumba za biashara (commercial real estate) hazina risk kubwa sana. Ndio maana mtu anakimbilia huko maana hata akikosekana mpangaji nyumba/frame itakaa mpaka apatikane mpangaji.

Ukifuga kuku au kulima cabbage ukikosa mteja week moja tu tayari hasara.

KIkubwa kwenye investment yoyote ni kusoma market ninche. Kuna uwekezaji una risk kubwa (ofcourse unakuwa na reward kubwa pia) na uwekezaji wenye risk ndogo na return yake huwa ni ndogo.

So waliochagua real estate wamewekeza kwenye low risk investment.

Kuna watu wanatupa hela hundreds of millions kwenye machimbo ya dhahabu kwa week halafu zinaungua chap tu na anarudi kesho yake na anaweza kutengeneza faida hata ya 100%.

Mtu mwingine angesema hizo millions bora ningejenga nyumba/frame niwe nakula kodi taratibu lakini mwingine anaona kama ni kupoteza muda anataka hizo millions zizae billions ndani ya mwezi na wapo wanaofanikiwa.

Kikubwa ni kujua uwezo wako na kuwa na strategies.
Oyaa ndawoo dogo mgerasi unashusha nondo kamili na kutema madini yaliyojitosheleza. Vipi mlishalima na kuvuna ngwara na dengu simanjiro? Mmemaliza pofu wote.
 
Watu wanapika na kuuza mbege tu kibamba tu hapo wana fanya maajabu unashangaa.

Kimara hapo wa rombo wana uza soup ya utumbo / mbuzi / mtori na goli la kuchoma mbuzi na ugali hela anayofunga daily utashangaa.

Kalieni frame za nguo tu 🤣🤣🤣
 
Mwanzoni sikuwa na exposure kabisa niliamini Frame ndio njia pekee ya kupata ukwasi, vijana wamefata mkumbo huo huo kijana ana mtaji wa million 5 anaenda kulipia Frame 1.5M per year anafatilia vibali laki 5 yote inaisha huko bado hajafanya decoration dukani mwisho anabaki na million 2.5 baada ya mwaka anafunga duka anaondoka?
Ukizunguka maeneo mengi hapa daresalam unakutana na duka mwaka huu wanauza nguo mwakani wanauza kitu kingine atleast yale maduka ya mangi yanaweza kutoboa hata miaka 5.

Mwanzo nilikuwa sijui kwamba hata kwenye ufugaji wa kuku unaweza kujenga nyumba na kupata premio, huko kwenye ufugaji nimeona watu wakipata some cash ambayo inawasaidia naona hawakimbizani na TRA na mlolongo wa tozo.

Kwanini watu bado tunakimbilia uchumi wa Frame? Je ni identity au ni nini?
Mambo yanayohusiana na kilimo na ufugaji kuna pesa. Hapo kwenye kilimo namaanisha baadhi ya mazao au uhifadhi wa mazao.

Kuna siku nilikaa nikawaza, AI imeleta mapinduzi ambayo yanatishia ajira za kada kadhaa zinazohusiana na utaalamu lakini nikaona yule atakayejihusisha na masuala ya kilimo na ufugaji ndiye atapiga pesa kwa sababu bado sana kwa Afrika, hiyo AI kuja kuzalisha mazao ya kilimo na ufugaji!
 
Kuna watu wengi TU vijijini na mjini wanaendesha Maisha Yao Kwa ufugaji peke yake na Maisha yanaenda, watasomesha ,watajenga na pia watalea familia Kwa huo huo ufugaji.
Nachokiona watu wanatamani kuiona hela ya kila siku ufugaji pesa inashikiliwa
 
Back
Top Bottom