Kwanini Tanzania tumeng'ang'ania uchumi wa frame za maduka? Mbona hata ufugaji unalipa?

Kuna uzi kama huu nilijibu kama hivi. Mtu anabeza retailers anasema watu wajikite kwenye uzalishaji. Sasa genius huyo anaewaona retailers hawana maono haoni kuwa akishazalisha atahitaji retailers kuuza bidhaa zake!
 
biashara ya viumbe vyenye roho ni risk sana. Nishashuhudia mtu akizika kuku zaidi ya 3000 kwa wakati mmoja .
Pamoja na hivo,hata kwenye makampuni Kuna kufilisika, kuachishwa kazi,mishahara kidogo nk.
Kwa upande wa kilimo, Kuna ukame, wingi wa mvua, na swala la soko pia.
Kwa hiyo kila pahala Kuna changamoto zake
 
Oyaa ndawoo dogo mgerasi unashusha nondo kamili na kutema madini yaliyojitosheleza. Vipi mlishalima na kuvuna ngwara na dengu simanjiro? Mmemaliza pofu wote.
 
Watu wanapika na kuuza mbege tu kibamba tu hapo wana fanya maajabu unashangaa.

Kimara hapo wa rombo wana uza soup ya utumbo / mbuzi / mtori na goli la kuchoma mbuzi na ugali hela anayofunga daily utashangaa.

Kalieni frame za nguo tu 🤣🤣🤣
 
Mambo yanayohusiana na kilimo na ufugaji kuna pesa. Hapo kwenye kilimo namaanisha baadhi ya mazao au uhifadhi wa mazao.

Kuna siku nilikaa nikawaza, AI imeleta mapinduzi ambayo yanatishia ajira za kada kadhaa zinazohusiana na utaalamu lakini nikaona yule atakayejihusisha na masuala ya kilimo na ufugaji ndiye atapiga pesa kwa sababu bado sana kwa Afrika, hiyo AI kuja kuzalisha mazao ya kilimo na ufugaji!
 
Oyaa ndawoo dogo mgerasi unashusha nondo kamili na kutema madini yaliyojitosheleza. Vipi mlishalima na kuvuna ngwara na dengu simanjiro? Mmemaliza pofu wote.
We kenge myebusi. Umbwaaa rudi Inshupu ukapalilie migomba mbusiiii
 
Kuna watu wengi TU vijijini na mjini wanaendesha Maisha Yao Kwa ufugaji peke yake na Maisha yanaenda, watasomesha ,watajenga na pia watalea familia Kwa huo huo ufugaji.
Nachokiona watu wanatamani kuiona hela ya kila siku ufugaji pesa inashikiliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…