Kwanini Tanzania tunapata watalii wachache kulinganisha na vivutio tulivyonavyo?

ishu sio namba ya watalii.. ishu ni mapato ya utalii, utalii wetu ni low density high quantity.. while kenya ni high density low quantity
Kwa hiyo tusijali sana watalii kua wachache? Hivyo hatuna haja ya watalii kua wengi kwa sababu sisi ni low density high quantity?
 

Kila sehemu tunafeli, huduma ni mbovu sana kuanzia airport
Wafanyakazi hawajali chochote kila kitu wanachukulia simple
Kweli tunatofautiana sana
 
Hilo la mda ndio baya zaidi yaani ndege ni huduma mbovu kuliko mabasi
Tuna shida sehemu nyingi sana
Watu hawataki kujifunza kwa wengine na ndio maana tunafeli kila sehemu
Ujuaji ni mwingi. Wakati ukienda Egypt kama tourist kwanza jamaa wa tour agent ndiye anakwenda immigration desk kuwaombea visa. Mkitoka nje mnakuta gari. Mnapelekwa hotelini mnapewa ratiba ya siku mnaachwa muoge na kurelax kidogo.
 
Sisi hatujali. Mtalii akijakuja tu tunamkamua kadri tuwezavyo. Ishu ya kurudi au kutokurudi kesho haituhusu.

Utashangaa watalii wanalalamikia gharama kubwa Tanzania na huduma mbovu. Pale waiting lounge ya Nyerere International Airport chips mayai TZS 18,000, unajiuliza haya mayai ya kenge au ya mbuni?

Ratings and reviews za hotel na huduma ni muhimu sana. Kama wanaandika ni chafu na haina maintanance unategemea nani ataenda kulala huko?
 
Chai andazi Sh15,000
 
Ujuaji ni mwingi. Wakati ukienda Egypt kama tourist kwanza jamaa wa tour agent ndiye anakwenda immigration desk kuwaombea visa. Mkitoka nje mnakuta gari. Mnapelekwa hotelini mnapewa ratiba ya siku mnaachwa muoge na kurelax kidogo.

Ni ujuaji wa kijinga sana na usumbufu. Egypt wako mbali sana kiutalii na mataifa yote yanatupita kwa mapokezi

Watalii wanaambiana katika mitandao na kutapika mabaya yote humo na wakisoma na kupeana habari hawakanyagi kabisa wanaona Bora waende Sharm-el-Sheikh wakanywe bia tu kuliko kuja kwetu
 
Hakimu Mfawidhi, Marketing strategy is poor, tume fail kwenye kutangaza vivutio vyetu vya ndani, ni mpaka tusaidiwe na kenya [emoji1139] kweli
 
Kuwekeza imewekeza vya kutosha shida ni moja tu ubunifu na mbinu katika kujitangaza
 
Kuwekeza imewekeza vya kutosha shida ni moja tu ubunifu na mbinu katika kujitangaza
Kuna standard coach zenye wahudumu kupokea watalii airport mpaka wakakokwenda?
Kuna affordable hotels za kutosha za mtu wa kawaida si zile za $3,000 kwa usiku?
 
Nimekwenda Cairo kama mtalii, usiku kuna dinner and dance kwenye boat ndani ya mto Nile, Kuna kupanda ngamia, kuona pyramid. Shamba la spice na maua. Ni vitu vidogo lakini vyote unawekewa kwenye ratiba. Na unaambiwa kesho saa nne mnakwenda kupanda ngamia. Sisi tunashindwa wapi?
 
Ukiuliza wahusika wa utalii kwanini tuna charge pesa nyingi hivi wanajibu sisi utalii wetu una target watakii matajiri tu, watalii maskini waende vi nchi vya huko jirani.

Unabaki unashangaa tu.
 
Kile kisiwa ambacho unapanda boat kutoka Slip Way. Ni location nzuri ukiandaa picnic kwa watalii, unaandaa snacks, chakula, vinywaji, DJ kuanzia saa nne asubuhi mpaka jioni mnawarudisha mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…