Kwanini Tanzania tunapata watalii wachache kulinganisha na vivutio tulivyonavyo?

Kwanini Tanzania tunapata watalii wachache kulinganisha na vivutio tulivyonavyo?

Hii channel ya Utalii sijui kwanini hatutangazi destination package Kama Thompson tv ya Uingereza ni kuiga content tuu.

Sisi tuna photojournalism tourism nzuri Sana lakini wanaozitangaza ni mpaka uone research Fulani huko Geographic channel na uulize zile image zilipitwa wapi unaambiwa. Selous au udzungwa.

Mfano huko Rubundo alipokwenda meko ni pazuri Sana Kama pangepatiwa promo.

Hakuna kitu kinatuangusha Kama mtalii anaongea hichi anapewa attitude Kama vile ni mswahili. Linalotufanya wengine tusitalii ndani ni attitude tunazopewa na waswahili wenzetu watoa huduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwezekana kuwe na boat za kuchukua watalii Dar kwenda Pemba kuona mashamba ya karafuu, jioni wanarudi Dar
 
Nimekwenda Cairo kama mtalii, usiku kuna dinner and dance kwenye boat ndani ya mto Nile, Kuna kupanda ngamia, kuona pyramid. Shamba la spice na maua. Ni vitu vidogo lakini vyote unawekewa kwenye ratiba. Na unaambiwa kesho saa nne mnakwenda kupanda ngamia. Sisi tunashindwa wapi?
Inafadhaisha,

Hakuna ubunifu au ubunifu ukiwepo unakutana na ukiritimba haieleweki..
Kwa bahari, mito, maziwa tuliyonayo, hatuna boat rides, hatuna hizo boat hotels za dinner,

Tupo tupo tu, tukitafuta mchawi! Too bad

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Tuache kufanya mambo kwa mazoea na tupunguze uswahili. Ikiwa tutafanikiwa kwenye hayo mambo basi mema ya nchi tutayafaidi.
 
Inafadhaisha,
Hakuna ubunifu au ubunifu ukiwepo unakutana na ukiritimba haieleweki..
Kwa bahari, mito, maziwa tuliyonayo, hatuna boat rides, hatuna hizo boat hotels za dinner,

Tupo tupo tu, tukitafuta mchawi! Too bad

Everyday is Saturday......................... 😎
Kuna wanaosema tumewekeza vya kutosha kwenye utalii. Fikiria hizo live band kwenye maji zitatoa ajira kwa vijana wangapi
 
Marketing strategy is poor, tume fail kwenye kutangaza vivutio vyetu vya ndani, ni mpaka tusaidiwe na Kenya [emoji1139] kweli
Hata ukitangaza huduma ni mbovu What do you expect?

Ingekuwa huduma zinaridhisha hao hao wachache wanaokuja wangeweza kuwa mabalozi kwa kuwashawishi jamaa zao ndugu zao, marafiki zao na hata majirani juu ya thamani ya pesa waliyoitoa na huduma waliyoipata.
 
Kuna wanaosema tumewekeza vya kutosha kwenye utalii. Fikiria hizo live band kwenye maji zitatoa ajira kwa vijana wangapi
Nchi hii tumewekeza kwenye siasa hilo halina ubishi wala mjadala, nenda kwa watendaji serikalini wengi wapo kisiasa..
Wanaishi kwa majungu na fitina na uzabizabina, hakuna weledi!

Tukipunguza uwekezaji kwenye siasa, tutasonga mbele!

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Ili sekta ya utalii ifanikiwe tunahitaji pia miundo mbinu. Unawapeleka watalii Ruaha au Mikumi kutoka JKN hakuna sehemu yenye hadhi njiani kwenye vyoo na maji ili watu wajisaidie na kunawa mikono. Kweli mnawaambia watalii wachimbe dawa bila maji wala tissues.

Hizi Break Points pia ziwe na petrol stations na migahawa anaetaka kula ale. Vyoo kwa watalii tour company iwalipie lakini wengine walipe sh 500 kutumia choo.
 
Kabla ujafika Morogoro ukitokea Chalinze Kuna maeneo mazuri sana kungetakiwa kuwe na hoteli nzuri sababu mandhari ya yale maeneo ni nzuri sana
 
Ili sekta ya utalii ifanikiwe tunahitaji pia miundo mbinu. Unawapeleka watalii Ruaha au Mikumi kutoka JKN hakuna sehemu yenye hadhi njiani kwenye vyoo na maji ili watu wajisaidie na kunawa mikono. Kweli mnawaambia watalii wachimbe dawa bila maji wala tissues.
Hizi facilities za kuchimba dawa ni shidaa

Walipaswa kuweka serviced, maintained clean stop points zenye hadhi huko, mbugani, haya masuala ya kuchimba dawa porini yabakie kuwa yetu sisi kama sisi..

Watalii wengine hawajawahi kutoka huko makwao, hawajui ulimwengu wa kuchimba dawa misituni!

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Kuna mzungu mmoja aliwahi kuniuliza mbona chips mayai mtaani ni 2,500 hadi 3,000 lakini Nyerere Airport ni 18,000. Kwa nini kuna tofauti kubwa hivyo na hizi za mtaani ni tamu sana?

Mtu kama huyo mnamjibu vipi?
Ukichunguza wenye tenda za hiyo migahawa wengi ni wachaga, hawa watu hawanaga utu kabisa wenyewe ni pesa mbele.
 
ishu sio namba ya watalii.. ishu ni mapato ya utalii, utalii wetu ni low density high quantity.. while kenya ni high density low quantity
Ndio argument tuliyokua nayo ila kiuhalisia hii hoja inakua valid pale ambapo demand ya products zetu inapokua kubwa kuliko carrying capacity yetu. Lakini mpaka sasa hivi bado tuko chini sana katika namba kulinganisha na vivutio vyetu.
 
ukiuliza wahusika wa utalii kwanini tuna charge pesa nyingi hivi wanajibu sisi utalii wetu una target watakii matajiri tu,watalii maskini waende vi nchi vya huko jirani.

Unabaki unashangaa tu.
Hii ndio sababu kuu.

Asilimia kubwa ya watalii tunaiwapokea Tanzania wanakuja kwa ajili ya kutembelea mbuga zetu pamoja na kupanda Mlima Kilimanjaro and Meru, Kwenda kwenye Fukwe na jufurahia hoteli zetu hizo ni ziada.

Tatizo ni kwamba gharama zetu (viingilio) ni vikubwa sana na hili limekuwa tatizo. Kama serikali ikiamua kutumia utalii kama sehemu ya kutoa ajira kwa wananchi hapo tutapokea mamilioni ya watalii.

Ila kama serikali itaweka kipaumbele kwa kukusanya mapato directly kutoka kwa mtalii hapo namba ya watalii lazima isue.
 
Mganga wa Binadamu anakuwa waziri Wa utalii unategemea apeleke strategic gani Kyle? Zaidi ya kubwabwaja twitter sijui nje ya box, na matapu tapu kibao.

Wanachokosea ni kudhani kuwa kila MTU anaweza kuendeleza utalii bila kujua kuwa ile ni professional na inahitaji taaluma ili kuweza kuboost na Ku maintain die destinations na kujua kuwa mnawatarget watu gani na je mtawapata?

Hasa ASA watalii wanaokuja TZ ni wale ambao wamemua mwenyewe kuna. Wachache sana wamekuja kwa sababu y nguvu ya Serikalini mikakati
 
Vichangiaji ni vingi, ila elimu isiyotosheleza ni tatizo sababishi la vyote. Inaanzia uwanja wa ndege. Panatakiwa pawe na wafanyakazi professionals wenye ukarimu na ujuzi wa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na lugha ya Kiingereza. SA na Kenya wametuzidi kwa kigezo hicho.

Ukifika nje ya jengo la uwanja wa ndege upate mpangilio wa kuridhisha wa teksi, na ziwe zinahudumiwa na watu wenye tabia nzuri, wasio wadanganyifu na wawe wanamudu Kiingereza vizuri.

Ukifika hotelini ukutane na wahudumu wenye ukarimu na elimu, na hasa wawe na uwezo wa kujibu maswali kwa Kiingereza.

Kama ni ufukweni basi ukitaka kuvinjari nje asubuhi usikutane na watu wasio na elimu ya utunzaji wa mazingira. Nilishakaa sana Kunduchi Beach Hotel na asubuhi nilikuwa naona wenyeji wengi wakitumia ufukwe wa bahari kama choo. Wanajisaidia aidha kwenye mchanga au ndani ya maji.

Mtalii gani atarudi au ataitangaza vizuri nchi ambayo watu wanarusha takataka za makopo yaliyokwisha soda nje ya mabasi au magari wanayosafiria?

Kwa waliofika Singapore wataweza kulinganisha na kuona ni ajabu kwamba tunaweza kuvutia hata hao watalii wachache. Ndugu zangu, tuko nyuma sana kwenye elimu.

Maendeleo ni Elimu na Elimu ni maendeleo
 
Mkiwapokea tu watalii Airport kuwe na coach linawasubiri. Wasio na viza passport zao zijisanywe na wafanyiwe fast track

Nje ya coach kuna mhudumu ana chupa baridi za maji au orange juice akiwa na tabasamu.

Wakifika hotelini wanapewa iteanary ya safari. Safari za kutwa wachukuliwe hotelini baada ya breakfast na kwenye safari kuwe na catering staff na chakula chao. Unaweza kuwa packed lunch au machalary, pilau na salad. Mchana mnahakikiasha wamepata lisaa la kupumzika pamoja na chakula na vinywaji. Kumbuka hawa watu wako likizo kwahiyo pombe ziwepo kila saa.

wakirudi hotelini jioni kuwe na dinner and dance.
 
Hii ndio sababu kuu.

Asilimia kubwa ya watalii tunaiwapokea Tanzania wanakuja kwa ajili ya kutembelea mbuga zetu pamoja na kupanda Mlima Kilimanjaro and Meru, Kwenda kwenye Fukwe na jufurahia hoteli zetu hizo ni ziada.

Tatizo ni kwamba gharama zetu (viingilio) ni vikubwa sana na hili limekuwa tatizo. Kama serikali ikiamua kutumia utalii kama sehemu ya kutoa ajira kwa wananchi hapo tutapokea mamilioni ya watalii.
Ila kama serikali itaweka kipaumbele kwa kukusanya mapato directly kutoka kwa mtalii hapo namba ya watalii lazima isue.
Kuna issue moja kubwa ambayo wahusika wanashindwa kuelewa hua wakiangalia Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar wanahisi zipo unique sana ila kiuhalisia they are not. Mfano mtalii akitoka Ulaya au America lengo lake kuu ni kuona Simba, Chuo, Tembo na wanyama wengine, ni wachache sana wanataka waone specific things kama Migration na other physical features.

Sasa ukiangalia competitors wetu Kenya, South Africa, Botswana, na Zimbabwe nao pia hawa wanyama wanapatikana. Similar case to Zanzibar kuna tropical Islands nyingi tu kama Mauritius, Seychelles na Comoros. At the end of the day Tanzania tuna unique attraction moja from the rest of the continent ambayo ni Kilimanjaro (Highest Peak in Africa ).

Wenzetu wametambua hilo wakawekeza katika Marketing, Pricing na Service. Sisi tumeng'ang'ana na uniqueness tu na kuhisi tupo special wakati kuna substitute destinations ambazo zinatoa same experience and at a reasonable price.
 
Back
Top Bottom