Wamepingana na Neno la Mungu
Ufunuo wa Yohana 22: 18. Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Acha kupotosha watu na kuharibu Neno la Mungu kwa kuchomoachomoa vifungu na kuvipatia maana unayoitaka wewe, kama vile imeandikwa leo au juzi biblia sio gazeti kwamba unaamka tu na kujipatia tafsiri..
hiyo ufunuo wa yohane 22:18-19. Haina maana kama unavotaka kutiaminisha hapa. Kajifunze historia ya icho kitabu cha ufunuo, mazingira ya uandishi wa icho kitabu cha ufunuo, kwanini kiliandikwa, mazingira na maisha ya walengwa wa icho kitabu nk.
Kukusaidia tu ni ivi:
ufunuo 22:18-19 inayohusu agizo la biblia la "usiongeze wala usipunguze neno".
ni ivi ndugu kipindi ivo vitabu vya biblia vinaandikwa hakukuwa na technologia ya uchapishaji au "copy and paste" kama ilivo leo. kumbe ili kupata copy ya kitabu (gombo) wao walichokuwa wanafanya ni ku-nakili kwa mkono, mikono yao ndio iliokuwa iki-nakili neno hadi neno, herufi hadi herufi mpaka kitabu kizima kinakamilika.
kazi hiyo ya kunakili ilikuwa inafanywa na watu maalumu waliojulikana kama "waandishi au waalimu wa sheria kwa jina lingine" (wanaitwa waandishi kwa sababu ya kazi hiyo ya ku-nakili maandiko ila kimsingi ndio hao walimu wa sheria).
kumbe basi baada ya kumaliza kunakili kitabu husika ilikujua kama kazi "nakala" HAIJACHAKACHULIWA, HAIJAONGEZWA WALA KUPUNGUZWA, HAINA MAKOSA(kama kukosea neno, kuruka au kusahau neno/herufi, nyongeza au upungufu wa maneno nk) walitafuta idadi ya maneno kwa kuhesabu neno hadi neno kisha walioanisha na idadi ya maneno kwenye gombo husika kama yana lingana au la. yakilingana basi iyo nakala inakuwa ni sahihi, idadi ikitofautiana hata kidogo basi iyo nakala inakuwa na mapungufu "au imeongezwa au imepunguzwa au ujumbe/maana imeharibiwa"
baada ya maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa ufunuo 22:18-19. hazina maana ya mantiki unayotaka kutuonesha hapo juu. ila waandishi wanataka kulinda na kutunza jumbe/unabii wa vitabu vyao usiharibiwe "usiongezwe wala usipunguzwe". huku kwetu leo tunaita hati miliki "copyright".
Zaidi kajisomee pia torati 4:2