Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania;
Kwanini TBC wanashindwa kununua mechi za Fenerbahçe watanzania wamuone Samatta?
Tulishindwa kununua mechi za Aston Villa kwa maana ligi kuu ya Uingereza inajuliakana kuwa ni aghali dunia nzima.
TANZANIA - TURKEY RELATIONS:
=====
JANUARY 2017: Rais wa Uturuki awasili nchini Tanzania na kupokelewa na maelfu ya watu katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Yasemin Eralp walikuwa mstari wa mbele katika mapokezi ya Rais Recep Tayyip Erdoğan. Majaliwa alimpokea Rais Erdoğan kwa niaba ya Rais John Magufuli.
Rais Erdoğan amepokelewa kwa ngoma za asili kama ishara ya utamaduni wa nchi ya Tanzania. Rais wa Uturuki amesema ataendeleza uhusiano mzuri na bara la Afrika na kuhakikisha kila nchi barani Afrika ina Balozi atakae iwakilisha Uturuki.
FEBRUARY 2017: Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki imeshinda zabuni ya kujenga reli ya kisasa (standard gauge) yenye urefu wa kilometa 300 kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro na njia za kupishana.
Ushindi wa zabuni hiyo umekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan kuitembelea Tanzania na mwenyeji wake, Rais John Magufuli pamoja na mambo mengine alimwomba aijenge reli hiyo.
Akizungumza jana wakati wa utiaji saini wa kandarasi hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), Masanja Kadogosa alisema zabuni ilitangazwa Septemba 9, 2016 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na tarehe ya kurudisha zabuni ilikuwa Desemba 6, 2016.
Kwa uhusiano huu mzuri uliopo baina ya Tanzania na Uturuki kwanini "lobbying" isifanyike kisha TBC wakaonesha mechi za Fenerbahçe tu?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.