Kwanini tende zinahusishwa na Uislamu?

Kwanini tende zinahusishwa na Uislamu?

Kivipi mkuu? Kwamba Waislamu wanitimia au hawaitumii?

Nafikiri, nyama ya kondoo na mbuzi hazitofautiani sana kwa ladha, ingawa watu wengi wanapendekea ya mbuzi.

Kuna baadhi ya watu hawapendi nyama ya kondoo, wanadai huwasababishia majipu.

Waislamu ndio wanatumia kwa mujibu wa huyo jamaa.

Niliambiwa haitumiki sehemu ambayo kuna kilevi.

So, wenye biashara ya nyama choma au bar hawanunui.
 
Hata vilemba na kanzu siyo mavazi ya waislamu, tatizo waislamu wanaupenda Uarabu, unaweza kwenda msikitini kuswali ijumaa ukiwa umevaa suti wala hamna shida yoyote.

Unaweza kwenda msikitini umelipuka pamba vile utakavyo wala haina shida yoyote, lakini mwislamu haliziki bila kuvaa mavazi ya Waarabu mikanzu na misuli.

Hata mjadala huu wa bandari na DP world ukiwahesabu wachache wanaotetea ukiacha wale waliokula rushwa hawa wengine wanatetea kwa sababu ya mahaba yao kwa Waarabu tu na wala hawana hoja yoyote.
Fahamu kwamba, waarabu Wana tamaduni zao, pia Kuna baadhi ya tamaduni za waarabu zinaingia katika uislamu, pia Kuna tamaduni za waarabu uislamu umezipiga vita

Hivyo uislamu una taratibu zake ambazo nyingine ni taratibu za waarabu hata wasiokuwa waislamu

Mavazi yanaingia katika dini ya uislamu

Vazi linalopendeza zaidi kwa waislamu ni kanzu na haya ni mafundisho

Japo haimaanishi mtu aaiyevaa kanzu ndio anapata dhambi au Ibada yake haikubaliki.
 
Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.

Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.

Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?

Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?

Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?

Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.

Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!

Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?
Kuna baadhi ya vitu vingine huwa vinahusishwa na dini fulani ila uhalisia sio

Mfano, Alkasusu ni kinywaji tu ambacho hutengenezwa na viungo vya kawaida tu ambavyo tunavitumia kila siku bila kujali dini

2. Kuna baadhi ya dawa za asilizinadhaniwa ni zinaitwa dawa za kisunnah, ila uhalisia ni dawa za mitishamba tu ambazo yoyote anaweza kutengeneza au kutumia
 
Ukimfuatilia Dr zakir yule kumkuta kavaa kanzu ni nadra sana ....

Unajua nn? kuna kitu kinaitwa sunnah yaani sio lazima ila unafuata yale ya mtume aliyofanya ...Mfano hizo tende mtume kama unajua enzi zake zilikuwa zinalimwa sana kwenye jamii yao wa waarabu sasa yeye alikuwa akitumia kufungulia(Ramadhan) ,basi hili tunda likawa kama kikokotezo yaani watu wanaiga ,haina shida kuiga ila mtizamo wa watu wanachukulia kweny dini ila mtu yeyote anaweza kula.

Kufuata sunnah ni njema sana ila unatakiwa kuwa na uelewa ili usilazimishe jambo maana sunnah ni bora ila sio lazima.

Jamii inatakiwa kusoma sana ili kutambua mambo ila mi nasali na suti mara kibao na hata wengi tunasali hivyo maana ni maeneo ya makazi wala hamna tatizo zote ni nguo .
Mara ya mwisho bilashaka nimevaa kanzu mwaka Jana! umeelezea vuzuri sana ila kiuhalisia na ukweli ni kwamba tu wasiokuwa waislam wanachuki sana na uislam the rest is blah blah tu.....

Kwasababu gani? Ngoja nieleze sababu chache kwa njia ya maswali

-tukivaa kanzu tunaambiwa tunaiga waarabu, ni kweli kwasababu asili ya kanzu ni vazi la middle east mpaka asia pia sio asili yetu sisi wapare na wadigo...Je suti asili yetu?? Kwanini suti, au trouser na shirt inaonekana kama ndio standards kwa jamii zetu Africa wakati pia sio mavazi yetu? Lini ushaskia humu ndani kumenongwa suti kuwa tunamuiga mzungu sio asili yetu?

Mjinga aweza fikiri kuwa nataka tuvae nusu uchi na vingozi maana ndio tunaambiwa walikuwa wakivaa hivyo our ancestors, hapana sina maana hiyo ila nilikuwa tu nataka kuibua hii double standard ambayo always ipo yaani kuna mambo ya jamii flani yakifutwa kwa baadhi ya watu kwao ndio standards/ vipimo wameweka vya ustaarabu ila ukifuata mambo ya jamii flani unaambiwa unaiga waarabu

Sasa mtu yua claim haswa kua kanzu na vilemba ni waarabu ila sisi waislam tunaiga tu, aya suti ni zao hao wahehe wanazozivaa makanisani??

Qur' an 3: 119

Ndio maana kuna kichaa mmoja kule Kenya anaitwa munish aliwahi eti kumdisi samia eti rais gani kila mahala ma ushungi hadi unajiuliza huyu mtu ana akili kweli

Na ukristo wenyewe baadhi ya sehemu kubwa ya mafundisho yao yamekuwa butu maana roll model wao nkubwa ni mzungu na wamekubali kuchanganyana sana uzungu na ukristo, Leo hii kuna baadhi ya watu wanaamini ukristo na uzungu ni sawa kumbe sio, pia kuna baadhi ya watu wanaamini ukristo umetokea uzunguni kumbe Abrahamic religion zote chimbuko lake ni hapo middle east ila Leo hii identity kubwa inatoka ulaya, kanzu pia ni vazi Leo lakini wanalinonga, wanaadisi ushungi ila watawa wale wanavaa, niliwahi kumuuliza mtu mkatoliki binti, kwanini watawa wanawake wanavaa kwa stara vile na nywele wanafunika ila nyie wengine hamfundishwi hivyo?? Nikamuuliza ni sheria gani zipo tu kwa watu specific ila watu wengine nyie sio lazima na wala hata hamuelekezwi na nyie mvae kwa stara namna ile na watu wote kwa mungu ni sawa isipokuwa wachamungu ndio wanadaraja kubwa zaidi kwake??

Hao jamaa wana double standards hatari kiufupi dunia huwa wanaona ni yao na Tanzania hii ni yao haha
 
Hata vilemba na kanzu siyo mavazi ya waislamu, tatizo waislamu wanaupenda Uarabu, unaweza kwenda msikitini kuswali ijumaa ukiwa umevaa suti wala hamna shida yoyote.

Unaweza kwenda msikitini umelipuka pamba vile utakavyo wala haina shida yoyote, lakini mwislamu haliziki bila kuvaa mavazi ya Waarabu mikanzu na misuli.

Hata mjadala huu wa bandari na DP world ukiwahesabu wachache wanaotetea ukiacha wale waliokula rushwa hawa wengine wanatetea kwa sababu ya mahaba yao kwa Waarabu tu na wala hawana hoja yoyote.

View: https://youtu.be/D2POHltursg
 
Kwenye orodha uliyoorodhesha inaonyesha dhahir kuwa nchi zilimazo tende nying NI zenye idadi kubwa ya waislam. Hivyo kusema tende ni chakula cha waislam ni Ile mazoea Tu
Sijaona sababu ya wewe kucomplicate Sana hili.

Je umewahi nunua tende ukaulizwa dini yako?

Hata miguu ya kuku na dagaa kuwa chakula chatu masikin haimaanishi kuwa matajiri hawali.
 
Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.

Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.

Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?

Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?

Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?

Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.

Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!

Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?
Mkuu Iko hivi, tende ni zao linalolimwa Sana uarabuni japo Kuna maeneo mengine zinalimwa Sana tu, Ila linahusishwa Sana na uislam kwa kuwa kwanza linalimwa Sana arabuni ambako ndio chimbuko la uislam, lakini pia katika mafundisho ya dini ya uislam yanatufundisha kuwa mara mfungaji atakapo kamilisha siku yake kwa kufunga anatakiwa chakula chale Cha kwanza kula iwe ni tende, kwa mantiki hiyo ndio maana inahusishwa Sana na uislam, lakini pia ukirejea katika Qur'an tukufu, Kuna Aya Allah anamwelekeza Maryam kutumia tende na hii ni katika kipindi Cha ujauzito wa nabii Issa alayhi salaam, Sasa ukichukulia hayo machache utaona ni kwa Nini tende inahusishwa Sana na uislam lakini ni chakula ambacho yeyote anaweza kutumia haijalishi ni muislam au si muislam.
 
Mara ya mwisho bilashaka nimevaa kanzu mwaka Jana! umeelezea vuzuri sana ila kiuhalisia na ukweli ni kwamba tu wasiokuwa waislam wanachuki sana na uislam the rest is blah blah tu.....

Kwasababu gani? Ngoja nieleze sababu chache kwa njia ya maswali

-tukivaa kanzu tunaambiwa tunaiga waarabu, ni kweli kwasababu asili ya kanzu ni vazi la middle east mpaka asia pia sio asili yetu sisi wapare na wadigo...Je suti asili yetu?? Kwanini suti, au trouser na shirt inaonekana kama ndio standards kwa jamii zetu Africa wakati pia sio mavazi yetu? Lini ushaskia humu ndani kumenongwa suti kuwa tunamuiga mzungu sio asili yetu?

Mjinga aweza fikiri kuwa nataka tuvae nusu uchi na vingozi maana ndio tunaambiwa walikuwa wakivaa hivyo our ancestors, hapana sina maana hiyo ila nilikuwa tu nataka kuibua hii double standard ambayo always ipo yaani kuna mambo ya jamii flani yakifutwa kwa baadhi ya watu kwao ndio standards/ vipimo wameweka vya ustaarabu ila ukifuata mambo ya jamii flani unaambiwa unaiga waarabu

Sasa mtu yua claim haswa kua kanzu na vilemba ni waarabu ila sisi waislam tunaiga tu, aya suti ni zao hao wahehe wanazozivaa makanisani??

Qur' an 3: 119

Ndio maana kuna kichaa mmoja kule Kenya anaitwa munish aliwahi eti kumdisi samia eti rais gani kila mahala ma ushungi hadi unajiuliza huyu mtu ana akili kweli

Na ukristo wenyewe baadhi ya sehemu kubwa ya mafundisho yao yamekuwa butu maana roll model wao nkubwa ni mzungu na wamekubali kuchanganyana sana uzungu na ukristo, Leo hii kuna baadhi ya watu wanaamini ukristo na uzungu ni sawa kumbe sio, pia kuna baadhi ya watu wanaamini ukristo umetokea uzunguni kumbe Abrahamic religion zote chimbuko lake ni hapo middle east ila Leo hii identity kubwa inatoka ulaya, kanzu pia ni vazi Leo lakini wanalinonga, wanaadisi ushungi ila watawa wale wanavaa, niliwahi kumuuliza mtu mkatoliki binti, kwanini watawa wanawake wanavaa kwa stara vile na nywele wanafunika ila nyie wengine hamfundishwi hivyo?? Nikamuuliza ni sheria gani zipo tu kwa watu specific ila watu wengine nyie sio lazima na wala hata hamuelekezwi na nyie mvae kwa stara namna ile na watu wote kwa mungu ni sawa isipokuwa wachamungu ndio wanadaraja kubwa zaidi kwake??

Hao jamaa wana double standards hatari kiufupi dunia huwa wanaona ni yao na Tanzania hii ni yao haha
Swadaqta!

Hata Dr sulley yule kumkuta kavaa kanzu ni nadra hizi ni sunnah wala hazina madhara yeyote ile ,ukivaa sawq usipovaa fresh ..
 
Kwenye orodha uliyoorodhesha inaonyesha dhahir kuwa nchi zilimazo tende nying NI zenye idadi kubwa ya waislam. Hivyo kusema tende ni chakula cha waislam ni Ile mazoea Tu
Sijaona sababu ya wewe kucomplicate Sana hili.

Je umewahi nunua tende ukaulizwa dini yako?

Hata miguu ya kuku na dagaa kuwa chakula chatu masikin haimaanishi kuwa matajiri hawali.
Mkuu utakuwa hujanielewa! Mimi si Muislamu lakini tende ni miongoni mwa matunda yangu pendwa.

Mtu kusema kuwa tende ni chakula cha Kiislamu, binafsi, naona ni imani potofu.

Swali langu lililenga kufahamu chanzo cha hiyo imani, na si kwamba na mimi ninaamini kama wengine wanavyoamini. Ila ningekuwa "mjinga", na mimi ningeweza kuamini hivyo.

Wewe huoni kuwa hiyo ni imani potofu?

Wewe huoni kuwa kuna watu wanajikosesha, pengine, virutibisho vizuri vilivyopo kwenye tende kisa imani potofu waliyouziwa kwenye gunia?
 
Hakuna Imani hapo , hayo ni mazoea tu
 
Duuh..! Kumbe MAREKANI NA U.S A nao wanalima tender? Daaah Hawa School na Shule hawa
 
Tanzania tende zinaweza kustawi wapi? Zinachukua muda gani hadi kuanza kuzaa matunda?
 
Hata mimi nashangaa kwani hata kahaba maarufu wa kwenye Biblia ni "Tamari" ambalo tafsiri yake ni tende.

Tena ni kahaba aliyehusishwa, ndani ya biblia, kuwa ni katika chanzo zhanzo cha uzazi wa Yesu.

Kahaba alitubu dhambi akawa mtu mwema,hata wewe ukiacha uchawa ukatubu dhambi ukawa mtu mwema utapata bwana.
 
maria alipomzaa yesu aliamrishwa ale tende lakini wakristo hawa wao ibada yao kwaya nyimbo hawajui dini yao ni ipi
 
Kwahiyo Maria ndio dini?
 
Attachments

  • FB_IMG_1692087231147.jpg
    FB_IMG_1692087231147.jpg
    29.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom