Kwanini tende zinahusishwa na Uislamu?

Kwanini tende zinahusishwa na Uislamu?

Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.

Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.

Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?

Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?

Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?

Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.

Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!

Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?
Wengi wao wanaochukulia hivyo ni wale waislam wasio na elimu, mtu amekariri tu dini na mambo ya kiarab lakini hajuwi lolote zaidi ya yale aliyokariri na wengi wako hivi hapa Tanzania. Ni hasara kubwa sana kwa taifa letu kuwa na watu wa namna hii kwa kweli.
 
Mi binafsi si muislam, napenda tende sana, huwa natamani ziwepo muda wote zinakouzwa nikanunue. Sina mipaka ya kula vyakula vinavyodhaniwa ni vya dini fulani. Hata suala la mahusiano ya kimapenzi sina mipaka, nikimpenda binti wa kiislam naye akinipenda imetoka hiyo, mwendo ni mapenzi motomoto. Avae kiislam aende msikitini poa tu, ninachojali ni utu na heshima. Imani ya dini hainuhusu
Mkuu mbona unamuangusha Mungu wetu wa kweli kipenzi chetu cha dhati YESU kwa kula matunda yenye mrengo wa kigaidi.

adriz
 
Nasubiri mtu ahusishe kitimoto na ukristo nilete evidence ya upande wa pili wanavyotuletea ushindani sokoni
 
Ulimbukeni unawaweka mbali na maendeleo duniani
Kuna tende nzuri sana zinaitwa Medjool hizi ni kubwa kuliko tende zingine na ni tamu sana ukila Tatu tu shibe

Wazalishaji walikuwa Morocco ila sasa wengi wanalima na kwa sasa nazinunua za South Africa hapa London box la 5kg ni £24.99 ( sh 75,000)
Hapo utajua SA hawana ujinga wa kuacha fursa

Nyie kalieni hayo hayo ooh tende za waislam wakati mpaka cake za tende zipo

Limeni mlete Ulaya
Nimesahau kumbe hamuwezi kwa uoga
Waswahili ni waoga wa biashara za nje
Bila kutoa bidhaa nje na kuwa na guts hamtoboi
Mazao yenu Bashe atapiga kelele sana na kuozea barabarani tu
 
Ukimfuatilia Dr zakir yule kumkuta kavaa kanzu ni nadra sana ....

Unajua nn? kuna kitu kinaitwa sunnah yaani sio lazima ila unafuata yale ya mtume aliyofanya ...Mfano hizo tende mtume kama unajua enzi zake zilikuwa zinalimwa sana kwenye jamii yao wa waarabu sasa yeye alikuwa akitumia kufungulia(Ramadhan) ,basi hili tunda likawa kama kikokotezo yaani watu wanaiga ,haina shida kuiga ila mtizamo wa watu wanachukulia kweny dini ila mtu yeyote anaweza kula.

Kufuata sunnah ni njema sana ila unatakiwa kuwa na uelewa ili usilazimishe jambo maana sunnah ni bora ila sio lazima.

Jamii inatakiwa kusoma sana ili kutambua mambo ila mi nasali na suti mara kibao na hata wengi tunasali hivyo maana ni maeneo ya makazi wala hamna tatizo zote ni nguo .
Mimi namsikiliza Ismail Ibn Musa Menk maarufu kama MUFT MENK wa Zimbabwe akili kubwa huyu

South Afrika Wakristo mpaka Mapastor wanamtumia kama refference
 
Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.

Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.

Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?

Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?

Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?

Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.

Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!

Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?
Tende inaliwa sana na Wakristo sikuhizi pengine kuliko Waislam

Zamani tatizo ilikuwa accessibility, ilikuwa ni vigumu kwa Mkristo kupata

Tende zilikuwa zinapatikana zaidi misikitini na wenye connections na Waarabu walikuwa wanapata kipindi cha Idd

Sikuhizi zinapatikana kila kona
 
Hata mimi nashangaa kwani hata kahaba maarufu wa kwenye Biblia ni "Tamari" ambalo tafsiri yake ni tende.

Tena ni kahaba aliyehusishwa, ndani ya biblia, kuwa ni katika chanzo zhanzo cha uzazi wa Yesu.
Nakurekebisha sio Tamari ni RAHABU, ni kweli Rahabu alikuwa na Undugu kwa mbali na Yesu kwasababu wote walikuwa ni wa Ukoo mmoja wa Daudi
 
Wengi wao wanaochukulia hivyo ni wale waislam wasio na elimu, mtu amekariri tu dini na mambo ya kiarab lakini hajuwi lolote zaidi ya yale aliyokariri na wengi wako hivi hapa Tanzania. Ni hasara kubwa sana kwa taifa letu kuwa na watu wa namna hii kwa kweli.
Ujinga ni mzigo
 
Mkuu mbona unamuangusha Mungu wetu wa kweli kipenzi chetu cha dhati YESU kwa kula matunda yenye mrengo wa kigaidi.

adriz
Tende ni chakula mkuu kama vyakula vingine. Hata Israel inalima tende. Tena, inashika nafasi ya pili kwa hicho kilimo.

NB. Taarifa hiyo nimeipata humu humu JF
 
Tende ni tunda tamu lenye faida nyingi, wavaa kobaaz kwa ubinafsi wao wanataka wafaidi wenyewe
 
Uturuki wameweza kujitofautisha kiasi kikubwa na utamaduni wa Kiarabu japo asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu!
Hata vilemba na kanzu siyo mavazi ya waislamu, tatizo waislamu wanaupenda Uarabu, unaweza kwenda msikitini kuswali ijumaa ukiwa umevaa suti wala hamna shida yoyote.

Unaweza kwenda msikitini umelipuka pamba vile utakavyo wala haina shida yoyote, lakini mwislamu haliziki bila kuvaa mavazi ya Waarabu mikanzu na misuli.

Hata mjadala huu wa bandari na DP world ukiwahesabu wachache wanaotetea ukiacha wale waliokula rushwa hawa wengine wanatetea kwa sababu ya mahaba yao kwa Waarabu tu na wala hawana hoja yoyote.
 
Hayo ya kuvaa kanzu yaliniponza ,bwana bwana si nilinunua kanzu yangu swaafi na kibaraghashia kama muuza alkasusu mashuhuri basi wife si kwa kununa kule kwa madai yake kuwa nimepata mwanamke muislam ndio najipendekeza huko[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.

Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.

Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?

Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?

Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?

Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.

Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!

Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?
Mara nyingi huwa sina imani na chakula ninachohisi muandaa ni mtu anayetaja kuwa kuna majini wasafi.
 
Back
Top Bottom