Kwanini tende zinahusishwa na Uislamu?

Wengi wao wanaochukulia hivyo ni wale waislam wasio na elimu, mtu amekariri tu dini na mambo ya kiarab lakini hajuwi lolote zaidi ya yale aliyokariri na wengi wako hivi hapa Tanzania. Ni hasara kubwa sana kwa taifa letu kuwa na watu wa namna hii kwa kweli.
 
Mkuu mbona unamuangusha Mungu wetu wa kweli kipenzi chetu cha dhati YESU kwa kula matunda yenye mrengo wa kigaidi.

adriz
 
Nasubiri mtu ahusishe kitimoto na ukristo nilete evidence ya upande wa pili wanavyotuletea ushindani sokoni
 
Ulimbukeni unawaweka mbali na maendeleo duniani
Kuna tende nzuri sana zinaitwa Medjool hizi ni kubwa kuliko tende zingine na ni tamu sana ukila Tatu tu shibe

Wazalishaji walikuwa Morocco ila sasa wengi wanalima na kwa sasa nazinunua za South Africa hapa London box la 5kg ni £24.99 ( sh 75,000)
Hapo utajua SA hawana ujinga wa kuacha fursa

Nyie kalieni hayo hayo ooh tende za waislam wakati mpaka cake za tende zipo

Limeni mlete Ulaya
Nimesahau kumbe hamuwezi kwa uoga
Waswahili ni waoga wa biashara za nje
Bila kutoa bidhaa nje na kuwa na guts hamtoboi
Mazao yenu Bashe atapiga kelele sana na kuozea barabarani tu
 
Mimi namsikiliza Ismail Ibn Musa Menk maarufu kama MUFT MENK wa Zimbabwe akili kubwa huyu

South Afrika Wakristo mpaka Mapastor wanamtumia kama refference
 
Tende inaliwa sana na Wakristo sikuhizi pengine kuliko Waislam

Zamani tatizo ilikuwa accessibility, ilikuwa ni vigumu kwa Mkristo kupata

Tende zilikuwa zinapatikana zaidi misikitini na wenye connections na Waarabu walikuwa wanapata kipindi cha Idd

Sikuhizi zinapatikana kila kona
 
Hata mimi nashangaa kwani hata kahaba maarufu wa kwenye Biblia ni "Tamari" ambalo tafsiri yake ni tende.

Tena ni kahaba aliyehusishwa, ndani ya biblia, kuwa ni katika chanzo zhanzo cha uzazi wa Yesu.
Nakurekebisha sio Tamari ni RAHABU, ni kweli Rahabu alikuwa na Undugu kwa mbali na Yesu kwasababu wote walikuwa ni wa Ukoo mmoja wa Daudi
 
Ujinga ni mzigo
 
Mkuu mbona unamuangusha Mungu wetu wa kweli kipenzi chetu cha dhati YESU kwa kula matunda yenye mrengo wa kigaidi.

adriz
Tende ni chakula mkuu kama vyakula vingine. Hata Israel inalima tende. Tena, inashika nafasi ya pili kwa hicho kilimo.

NB. Taarifa hiyo nimeipata humu humu JF
 
Tende ni tunda tamu lenye faida nyingi, wavaa kobaaz kwa ubinafsi wao wanataka wafaidi wenyewe
 
Uturuki wameweza kujitofautisha kiasi kikubwa na utamaduni wa Kiarabu japo asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu!
 
Hayo ya kuvaa kanzu yaliniponza ,bwana bwana si nilinunua kanzu yangu swaafi na kibaraghashia kama muuza alkasusu mashuhuri basi wife si kwa kununa kule kwa madai yake kuwa nimepata mwanamke muislam ndio najipendekeza huko[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mara nyingi huwa sina imani na chakula ninachohisi muandaa ni mtu anayetaja kuwa kuna majini wasafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…