Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 289
- 415
MBEYA KUMENOGA HASWAAA
Leo ndiyo ile siku ambayo uchaguzi wa chama Cha soka mkoa wa Mbeya ulitakiwa kufanyika.
Asubuhi majira ya saa tatu kulitakiwa kuwa na kikao Cha kamati Tendaji lakini baadhi ya wajumbe ambao wako upande wa Elias Mwanjala wakagoma kuingia Kwenye kikao hicho Cha kamati Tendaji.
Baadae majira ya saa nne na nusu Katibu wa Cha Cha mpira mkoa wa Mbeya LUCAS KUBAJA akawaita wajumbe FAKE ili kuingia Kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi.
Na kuwaacha nje wajumbe halali waliyochaguliwa Kwa mujibu wa katiba mpya iliyosainiwa na BMT.
Wakati yote hayo yanaendelea nje kulikuwa na Gari ya Polisi ambao wamebeba mabomu ya machozi.
Baada ya kuingia wajumbe FAKE Ukumbini, Mwenyekiti anaye maliza muda wake SADICK JUMBE aligoma kufungua mkutano huo kutokana na kuwepo Kwa wajumbe FAKE.
Mwenyekiti alipogoma kufungua mkutano huo ndipo Afisa michezo wa mkoa wa Mbeya ROBERT MFUGALE akaihoji kamati ya uchaguzi ya TFF kuhusiana na Sintofahamu hiyo,kamati ikakiri kuwa Kuna makosa yamefanyika ila hawawezi kuahirisha uchaguzi maana wako nje ya muda,hivyo ni lazima uchaguzi ufanyike.
Afisa michezo akagomea zoezi la uchaguzi kufanyika na kutoka nje ya ukumbi wa mkutano.
Naye mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu TFF , Mohamed Mashango akaamua kujitoa Kwenye uchaguzi huo kutokana kuwa batili.
Huyu Elias Mwanjala amekuwa tatizo kubwa sana maana kila Chaguzi amekuwa akienda kinyume na Katiba Kwa kulazimisha mambo huku akiirubuni kamati ya uchaguzi.
Naye katibu wa chama Cha mpira mkoa wa Mbeya LUCAS KUBAJA amejigeuza mwenyekiti hivi Sasa maana kila jukumu analibeba yeye na kupelekea kuleta Sintofahamu mkoani Mbeya.
Taarifa zilizipo mpaka Sasa nikwamba wajumbe FAKE wamempitisha ELIAS MWANJALA kuwa mwenyekiti.