Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania eti;
Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na ukubwa wa engine ya chombo (CC-Cubic Centimetres) kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara wa mtumishi?
(1) Kwanini gari kama IST pamoja na Landcruiser V8 yote yakitenda kosa moja la usalama barabarani kama vile overspeeding wanalipa tozo inayofanana ya 30,000/=?
(2) Mbona mfanyakazi anayepokea mshahara basic wa 1,500,000/= pamoja na mwingine anayepokea 300,000/= wanalipa viwango tofauti vya kodi ya PAYE?
(3) Katika kuvuka daraja la Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wanalipa kulingana na ukubwa wa gari na kwanini hakuna tozo za kufanana?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.