Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Hapo nadhani hakuna mzani ndio maana iko Flat rate ya 30000; Inawezekana wameangalia uwezo rafiki wa wamiliki magari wengi wastani ukaangukia hapo (sina hakika kigezo gani walitumia, inawezekana waliamua tu)
Okay...
 
Kumbuka hizi tozo hazikuwekwa ili kuwa sehemu ya chanzo cha mapato ma serikali waliweka tozo ili iwe onyo kwa muhusika pale anapokosea .

Ila kwa serikali hii ilipofikia kila sehemu yenye kuingiza hela wao wanataka iwe sehemu ya kuingiza mapato serikali kuu.
 
Kumbuka hizi tozo hazikuwekwa ili kuwa sehemu ya chanzo cha mapato ma serikali waliweka tozo ili iwe onyo kwa muhusika pale anapokosea .
Kwanini Murder na Manslaughter yote ni mauaji lakini yana hukumu mbili tofauti?...
 
Yaani Kosa halijapimwa, ndio maana fine yake ni moja; Kosa likiwekwa kwenye mizania basi nadhani hapo fine zitaanza kutofautiana. Fine haiitaji kupimwa, maana inategemea zaidi Kosa lililopimwa ili fine yenyewe iwe Applied.
Sawa mkuu
 
Ili kuweka records sahihi, maana madereva wengine huiba magari yard na kwemda kupiga day worker bila kumtaarifu bosi, hivyo lazima tujue aliyekuwa anaendesha
Aliyekuwa anaendesha ina umuhimu gani kama jina la mmiliki tayari lipo TRA? Hii justification yako haina mashiko hata kidogo mkuu
 
Katika kuvuka daraja la Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wanalipa kulingana na ukubwa wa gari na kwanini hakuna tozo za kufanana?
Kwenye daraja wanaangalia uzito wa gari na sio kosa. Faini ya barabarani inalipwa kutokana na kosa na si uzito au bei ya gari. Kosa linamhusu dereva na sio gari hivyo fine inawekwa kwa kukosea kwa dereva mfano kutokusimama kwenye zebra, kupita taa nyekundu, kutovaa mkanda n.k
 
Lakini si kweli pia kwamba bajaji aliyebeba abiria akavuka redlight na akagonga na lory ataua watu wengi zaidi ya Lorry la mchanga likivuka redlight na akagongwa na Lorry ambapo mafereva wote wanauwezekano mkubwa wa kupona? Kwahiyo ukubwa wa engibe sio kigezo consistent na hakiqualify kuwa base of reference
Kosa ni kusababisha ajali. Wakianza kuangalia impact itakuwa ngumu kupanga fine. Inaweza ikavuka bodaboda na ikasababisha daladala kuikwepa na kupinduka na kuua watu kumi Sasa hapo utasemaje kuhusu udogo wa bodaboda?
 
Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?
Yale unayolipishwa njiani ni makosa madogo kwa mujibu wa sheria. Makosa makubwa yanatakiwa yatolewe hukumu mahakamani na unaweza hata kufungwa miaka 10. Mfano dereva aliyesababisha ajali ya Sokoine alifungwa miaka 15 jela.
 
Kuna kosa la barabarani likawa la ugaidi mfano kugonga kwa makusudi msafara wa kiongozi
 
Back
Top Bottom