Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Tofauti iko kwenye majina na dhana yake.

Payee(tax) v/s Fine .

Moja ni kodi inalipwa na kila MTU, moja ni adhabu inalipwa na mtenda kosa vitakuwaje sawa?
 
Reactions: Ccc
Haiwezekani, sababu kama barabara ni moja kwa magari ya aina zote...

Kama ni taa za kuongozea magari ni moja kwa magari ya aina zote...

Kama ni zebra crossing ni moja kwa magari ya aina zote...

Kama ni round about ni moja kwa magari ya aina zote...

Kama ni madaraja hayo hayo hupitisha gari za aina zote...

Faini za makosa barabarababu kwa nini zitofautaine?



Cc: mahondaw
 
Basi hata mtu akifanya kosa la kukwepa kodi, aangaliwe umri wake kwenye kushughulikiwa.
Ndio maana hata mahakamani huwa mtuhumiwa hupewa nafasi ya kujitetea baada ya kukutwa na hatia ili mahakami impunguzie adhabu. Wengi wao husema kwamba wana mke na watoto wanaowategemea hivyo mahakama pamoja na wazee wa baraza kuwa na huruma nao
 
Athari za makosa hazijalishi ukubwa wa makosa mfano ajali.
Anayegongwa na Lorry na anayegongwa na Bajaj zote zikiwa katika speed sawa, ni nani yupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha?

Bajaj na Lorry zikigongana na IST kwa speed sawa na nyakati tofauti impact zake zitafanana?
 
Anayegongwa na Lorry na anayegongwa na Bajaj zote zikiwa katika speed sawa, ni nani yupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha?

Bajaj na Lorry zikigongana na IST kwa speed sawa na nyakati tofauti impact zake zitafanana?
Issue sio athari mkuu. Issue ni kwamba wote wanakuwa na kosa la uzembe. So uzembe ndo unapelekea penalt inayofanana.
 
Issue sio athari mkuu. Issue ni kwamba wote wanakuwa na kosa la uzembe. So uzembe ndo unapelekea penalt inayofanana.
Katika kuvuka daraja la Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wanalipa kulingana na ukubwa wa gari na kwanini hakuna tozo za kufanana?
 
[emoji1540][emoji1540][emoji1540][emoji1540]

Assuming magari yanaenda at same speed, wewe uko na ki corolla chako halafu ukagongwa na Vitz Vs kugongwa na Cruiser lenye ngao, will it be the same?
 
Hyo ni faini kwa dereva na sio gari MZEE,kule kwa nyerere au kwenye mizani wanaangalia uzito Wa chombo...labda ungesema kwa nini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake ILI kuendana na hiyo PAYE ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa
Au sio MZEE infant,
 
labda ungesema kwa nini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake ILI kuendana na hiyo PAYE ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa
Au sio MZEE infant,
Sawa mkuu, mimi huwa sikubaliani kabisa na hii dhana ya kulipa flat rate kwa makosa yote ya barabarani
 
Gari halifanyi makosa ya usalama barabarani. Dereva ndiye anayefanya hayo makosa. Kwa hiyo adhabu ni hiyo hiyo moja uwe unaendesha lori, Toyota Landcruiser, Bus, VW Polo, Mark II, n.k. Ikija kwenye kivuko, gari ndilo linalovukishwa. Hivyo ushuru utategemea uzito wa gari.
 
Kwa sababu ukubwa wa madhara ya kuvunja sheria hizo ni yale yale bila kujali ukubwa wa engine. Ukivuka redlight na ukasababisha ajali watu wanakufa na wabaweza wakafa wengi zadi kwenye gari ya engine ndogo kuliko lorry kubwa la mizigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…