Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Yani kuna ugumu gani wa kazi kwenye hili shirika? Maana anayeanza kazi tu anakomba mpaka million tano kwa mwezi. Ni mshahara wa mwaka mzima wa mwalimu.

Inamana kazi yao inaendana na kiwango cha mshahara? Dogo kaingizwa juzi tu kimagumashi hana hata miaka mitatu tayari kashusha Prado mpya zero kilometer pale Port. Nishauri serikali siyo nawaonea donge, ila wajaribu kupunguza hiki kiwango, haiwezekani mshahara wa mwalimu yeye anapiga kwa siku moja tu.

Nataka kujua kwa lipi hasa mpaka wapewe pesa ndefu kiasi hiki, yani unakaa miaka mitano tu kazini tayari salary slip inasoma million nane [emoji849].

View attachment 2443725
Jamaa huwezagi kuandka mada zako bila kutaja walimu
 
Itakuwa na yeye mwalimu anatumia jukwaa kutaka mabadiliko maana kuacha kazi anaogopa .same to me kipindi jobless niliilaumu sana serikali now shavu kimyaaa hata kutetea vijana wenzangu mtihani

Cc @mwifa
Siwezi kuwa abadani
 
Kwani usihoji sehemu nyingine wapewe mishahara kama ya TPDC au na wewe unataka watu wanaoishi kama malaika waje waishi kama mashetani. Iyo mishahara ya TPDC ndo iwe scale kwa sector nyingine wajifunze kulipa watu vizuri.
 
Nilifanya kazi TPDC enzi Mkurugenzi Mkuu akiwa Yonna Kilagane,Mwenyekiti wa Bodi alikuwa General Mstaafu Robert Mboma,Mkurugenzi wa Masoko akiwa Dismas Fuko, Mkurugenzi wa Exploration Halfan Halfan ambaye baada ya kustaafu Mama Samia kamteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC hapohapo,enzi Ofisi zipo Upanga kabla hatujahamia Mkapa Tower.
Uzuri wa TPDC upo kwenye kuwajali wafanyakazi wake kitaaluma,maana ukipelekwa kusoma Masters au PhD Ulaya unalipwa mpaka Pesa ya Pedi inakuwa kwenye Bajeti yako.Wakati huo Eng.Modestus Lumato alikuwa Ofisa wa kawaida na sasa hivi ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,wakati Eng.Charles Sangweni alikuwa Ofisa wa kawaida na sasa hivi ni Mkurugenzi Mkuu wa PURA.
Bwana MPWAYUNGU uliza swali lolote kuhusu TPDC nitakujibu
 
mzee hawakuelewi hata kidogo, ule msosi wa mchana pekee niliogonga pale, unazidi 50k wallahi

na hao jamaa daily wanakula ivyo

jamaa wapo kwenye bahari ya asali
Mashirika ya umma watu wanakula vinono. Mambo ya kawaida tu. Tuendelee kupambana katika harakati zetu za kimajinuni tuwafikie hakuna namna
Tuwakatie denge kwenye mishe zetu
 
Nilifanya kazi TPDC enzi Mkurugenzi Mkuu akiwa Yonna Kilagane,Mwenyekiti wa Bodi alikuwa General Mstaafu Robert Mboma,Mkurugenzi wa Masoko akiwa Dismas Fuko, Mkurugenzi wa Exploration Halfan Halfan ambaye baada ya kustaafu Mama Samia kamteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC hapohapo,enzi Ofisi zipo Upanga kabla hatujahamia Mkapa Tower.
Uzuri wa TPDC upo kwenye kuwajali wafanyakazi wake kitaaluma,maana ukipelekwa kusoma Masters au PhD Ulaya unalipwa mpaka Pesa ya Pedi inakuwa kwenye Bajeti yako
asali ilikuwaje mzee ha ha
 
Back
Top Bottom