Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Mfano:-
  • Una 100,000/= unataka uigawe kwa watoto wako 100 (walimu); kila mtoto atapata 1,000
  • Mtu mwingine naye ana 100,000, akaigawa kwa watoto wake (25); kila mmoja atapata 4,000
Hii inamaanisha wingi wa wafanyakazi, unapunguza mgao wa kila mmoja.
 
Pia udereva una madaraja hauwezi kufananisha maslahi ya VIP na PSV.
 
Nakukubali sana jembe langu mpwayungu village . Riziki hupangwa na Mungu na wala usisikitike fulani anapopatwa na mazuri, wala usifurahi fulani anapopatwa na mabaya.
 
Wewe kweli ni muandamizi Enzi hizo hata sisi tuliofanya field hapo tulikuwa tunapewa vijisenti
 
Okay..

Huko ukiwaambia nchi ngumu hawakuelewi..wanakuona umechanganyikiwa maana asali ni ya kutosha
Kabisa kiongozi Kuna jamaa angu yupo pale wizara za madini nianag'aa kama diamond anamatumizi ya hovyo minimum Kwa siku sio chini ya laki tano mpka Sita, yani hiyo pesa ni every day
 
Namba sita hapo wenye hela ni watu wa certificate na diploma imagine na degree yangu ya electric natumia harrier ambayo niliuziwa na shemeji yangu kwa milioni 8 (ni kama alinipa tu) ila kuna dogo wa operation Ana diploma Ana prado [emoji3]

So unaweza kupata kwenye mamlaka lkn bado ukawa njaa kali tu

Kuna jamaa anafanya kazi LITA Ana uhakika wa kukunja laki kila siku

•Jamaa wa ikulu asiponipeleka MSATA nitamloga
 
Mzee Mpwayungu hii dunia haina usawa. Cha muhimu ni kupambana tu usikose basic needs. Waalimu kwa kweli wana wakati mgumu. Hela yao ni ndogo ila ukirudi nyuma utaona wengi wao hawakufanya vizuri form 4 au 6 tofauti na waliosoma Petroleum Engineering. Hiyo kozi inachukua vipanga tupu waliosoma sayansi wakati hata division 3 ya 13 unaweza ingia Education UDSM. Kingine pia ajira za hao watu ni chache hivyo kitendo cha kwenda kusomea Petroleum Engineering walichukua risk kubwa mno. Ikumbukwe hata kwenye biashara sehemu yenye risk kubwa ndo kuna hela kubwa.

Waalimu pia wanafaidika na muda mwingi wa likizo kwenye mwaka. Ile miezi wanafunzi wanayofunga pia automatically waalimu wanapata likizo tofauti na fani zingine. Nawashauri waalimu wasikate tamaa wajiongeze kwenye ujasiriamali maana muda wa ziada wanao mwingi. Pia wasikae mbali na Chama Cha Mapinduzi kwasababu nyakati za uchaguzi wanawapaga madili.
 
Sawa, nikwavigezo gn walivyozingatia kuwapa mshahara mkubwa wafanyakazi wake, maana naona kama hiyo ni oversalary
 
kuna watu Tanzania ni watumishi wa umma na wengine humo humo serikalini ni kama deiwaka tuu sio sawa kabisa kuna taasisi wameshia wekewa mpunga wa mwisho wa mwaka huko halmashauli ni mwendo wa salary to salary
Naishangaa sana serikali haijui kuwa maisha yamebadilika, kumlipa mwalimu laki tano Kwa maisha ya sasa ni fedheha, lakini unakuta mtu yupo TPDC anagongwa million 7 Sasa unajiuliza Hawa wanapewa pesa ndefu hivyo wana hadhi kiasi gani cha kumpita Mara kumi mtumishi wa halmashauri
 
Mfano:-
  • Una 100,000/= unataka uigawe kwa watoto wako 100 (walimu); kila mtoto atapata 1,000
  • Mtu mwingine naye ana 100,000, akaigawa kwa watoto wake (25); kila mmoja atapata 4,000
Hii inamaanisha wingi wa wafanyakazi, unapunguza mgao wa kila mmoja.
Yeah sure, bora umelitambua hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…