Nilifanya kazi TPDC enzi Mkurugenzi Mkuu akiwa Yonna Kilagane,Mwenyekiti wa Bodi alikuwa General Mstaafu Robert Mboma,Mkurugenzi wa Masoko akiwa Dismas Fuko, Mkurugenzi wa Exploration Halfan Halfan ambaye baada ya kustaafu Mama Samia kamteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC hapohapo,enzi Ofisi zipo Upanga kabla hatujahamia Mkapa Tower.
Uzuri wa TPDC upo kwenye kuwajali wafanyakazi wake kitaaluma,maana ukipelekwa kusoma Masters au PhD Ulaya unalipwa mpaka Pesa ya Pedi inakuwa kwenye Bajeti yako.Wakati huo Eng.Modestus Lumato alikuwa Ofisa wa kawaida na sasa hivi ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,wakati Eng.Charles Sangweni alikuwa Ofisa wa kawaida na sasa hivi ni Mkurugenzi Mkuu wa PURA.
Bwana MPWAYUNGU uliza swali lolote kuhusu TPDC nitakujibu