Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Hizi za TPDC na PURA zinazotangazwa PSRS je? Idhini si imetoka kwao? maana mwajiri ndio anapeleka maombi PSRS
 
Kila taasisi au shirika la serikali lina ajiri kupitia PSRS, hawa TPDC si kazi zao zilitangazwa huko utumishi hivi karibuni?
Labda kama wameanza siku za karibuni kupitia PSRS,lakini muda mwingi walikuwa wanaajiri wao direct,na si kweli kwamba kila Taasisi/Shirika la Serikali linaajiri kupitia PSRS,leo hii TANESCO wametangaza nafasi 5 au 6 lakini maombi unatuma kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO direct na sio PSRS
 
Hizo hapo,maombi ni direct kwa Mkurugenzi Mkuu TANESCO
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji120][emoji120]
 
Dah, watu wanakula maisha ahse. Maninaa
 
Mmmh,Watu Wana enjoy mema ya nchi
 
mkuu na mimi huwezi kunifanyia mpango nmesoma electrical nna upper second Ila npo tu kitaa nasugua benchi
 
Umetaja hadi majina duh 😃
 
ila mishahara ya Tanzania inatakiwa kufanyiwa review watu wote mna degree moja mfano accounts ya halmashauli analipwa kidogo wa TRA au Bot au TCRA anampita mara kumi hii sio sawa wakati nature ya kazi ni moja
Hayo mashirika kama TPDC ni wazalishaji wakati halmashauri ni walaji, so hawawezi kuwa sawa na ni haki yao kulipwa hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mishahara ya namna hii ni balaa na ni mitamu

Hyo 5 mil mwalimu anahangaika kuikopa bank na mpaka anamhonga afisa mikopo,afu kuna dogo anaikunja kwa mwezi na class alikuwa wa kawaida tu,
Elimu wanalingana?

Masomo waliyosoma yanalingana ugumu?

Kuna masomo huyo mwalimu mwenyewe aliyakimbia hata digrii akiambiwa kachukue hii wako wachache akakimbia mbio kuwa mimi siwezi

Pili huyo wa TPDC akitishia kuacha kazi na mwalimu akitishia kuacha kazi serikali itataka kumbembeleza yupi asiache kazi mwalimu au huyo mtaalamu wa TPDC?

Kupima kazi ipi muhimu waambie wote waandike barua ya notice masaa 24 kuacha kazi uone nani atajibiwa haraka kuwa kwenda zako.Mwakimu atakuwa wa kwanza kujibiwa kuwa ombi lako limekubaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…