Candela
JF-Expert Member
- Aug 12, 2021
- 935
- 2,553
Unaenda Brela unafungua kampuni kwa kupeleka documents zote, unafika TRA kuchukua TIN Cert wanataka tena Documents ulizopeleka Brela.
Wakati huo tayari mfumo wa Brela umewataarifu kuwa kuna Kampuni mpya imesajiliwa na TRA wanakupa TIN namba automatic.
Sasa najiuliza TRA hawana imani na Brela mpaka waombe document mara 2? Kwani wanashindwa ku-link tu wakaziona kutokea Brela kama ambavyo wanalink ufunguaji wa kampuni.
Yaani wananikumbusha Taasisi kama Idara ya Uhamiaji, wao ndio walikukagua ukapewa NIDA ila ukienda kuomba passport na NIDA hawaitambui wanataka upeleke nyaraka sawa na ulizopeleka wakati unaomba NIDA. Huwa sielewi aisee.
=====================
MAJIBU YA BRELA

Habari, zoezi la kufungua kampuni ni rahisi na ufanyika kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wetu wa ors.brela.go.tz, pindi unapojaza taarifa za usajili wa kampuni yako na kukutana na changamoto usisite kuwasiliana nasi kupitia namba yetu ya kituo cha miito BRELA 0222212800 kwa msaada zaidi.
wengi wanatamani kufungua kampuni ila mchakato haupo rafiki,
Usajili wa kampuni unafanyika moja kwa moja kwa njia ya mtandao kupitia BRELA ORS au http://www.brela.go.tz, unatakiwa kuwa na:- 1.Katiba ya kampuni (Memorandum and Articles of association) 2.Namba ya kitambulisho cha taifa (NIN) kwa wahusika ambao ni watanzania kwa wahusika ambao sio watanzania wanatakiwa kuwa na hati ya kusafiria (passport) 3.Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) kwa wakurugenzi ambao ni watanzania 4.Barua pepe kwa wahusika wote 5.Namba ya simu ya kila muhusika 6.Fomu ya maadili utaipata katika mfumo wetu...NATAKA NIFUNGUE KAMPUNI
NIPE DARASA ZAIDI.