Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

NHIF ndiyo sababu Hospital nyingi kuendelea kuwepo, bila NHIF hospital nyingi zitakufa
 
Sasa sms inakuja baadae!kifupi Kuna ubabaifu mwingi
Kwaujumla hali ndivyo ilivyo, wizi kila sehemu. Ila hata kama ni baadae, wewe ukiona kunawasiwasi toa taarifa. Nchi yetu sote hii.
 
Ili huu mfuko uweze NHIF yatakiwa izingatie hilo swala.
Kwamba hospital lazima impe mgonjwa karatasi za matibabu
Hospital impe mgonjwa bill aisome ndio aweke saini
Mgonjwa atumiwe meseji na NHIF kuhusiana na bill yake
Nimekuelewa mkuu!
 
Kwaujumla hali ndivyo ilivyo, wizi kila sehemu. Ila hata kama ni baadae, wewe ukiona kunawasiwasi toa taarifa. Nchi yetu sote hii.
Mmh unahamisha ulaji to from one place to another
 
Na huu ndiyo ukweli...

Kinachoshangaza ni kuwa tunaoliongelea hili ni sisi tunaolipiwa na bima ambayo yenyewe imetulia tuli!

Wakiona unawagusa gusa huko, wanatokea na matusi na vitisho juu kuwanyamazisha watoa hoja.

Hii nchi ni ngumu sana.
 
Mfano, Agha Khan hawapokei NHIF Kwasababu ni kibima takataka kabisa
Yeah, maana kama Wagonjwa wenyewe ndio Hawa, Bure kabisa
Ila wanapokea zile special NHIF kama za wabunge, TRA, BOT, NMB na the likes, hizi za tupate sote hawazitaki.
Ila kwenye polyclinic wanapokea zote
 
NHIF ukiwaedekeza Kama una kakituo kako, utafirisika asubuhi tu.

Mfano:

Kidonge Cha Paracetamol, wao wanalipa Tsh 20 kimoja.

Magnesium, Chlorpheni Tsh 10 kwa kidonge.

Wound dressing/stitches Tsh 2000.

Na bado ukitoa huduma nusu ya Pesa utakadai ITAKATWA utapewa nusu kwa vijisababu kibao.

Sasa ukikomaa nao, ndani ya miezi 6 tu utajikuta hata pesa ya KULIPA DAWA au kulipa wafanyakazi HUNA.
Mkuu, hapa utapoteza nguvu zako kujibizana na watu wasioelewa hata wanachokitaka
Wamekazana kudai risiti na kufungiwa mahesabu utadhani ndio walichokifuata hospital
Hawajui hata namna gani Hawa NHIF jinsi wanavyosumbua kulipa madai ya Huduma ya wanufaika wao
Mijitu imeshupaza shingo humu
Sijui wangekua na Bima kama strategies au assemble wangekuaje
Fukara ni Fukara tu, ndio maana NHIF wanawakomoa kwa kuwapa dawa cheap wakapambane mbele
 
Hyo ni agha khan ya wapi...au Peponi huko. Acha kusikiliza radio mbaoo.. me ni mwaka agha khan tunapokea hyo bima bila shida.. ni moja ya Bima inayotupa pesa nyingi
Kule Dar main campus wanapokea fast track only ambazo ni BOT, NMB, TRA, CRDB na mfano wa hizo
Polyclinic ndio wanapokea wanahudumia mpaka hizi za kawaida
 
Kule Dar main campus wanapokea fast track only ambazo ni BOT, NMB, TRA, CRDB na mfano wa hizo
Polyclinic ndio wanapokea wanahudumia mpaka hizi za kawaida
Yaani ndio ujinga ni mtaji mkubwa sana.

Yaani mtu anadhani Adui yake ni vituo vya Afya na hao NHIF ndio wanaompenda na kumjali kinoma😂
 
Binafsi sijawahi kupata. Napeleka sana wanangu na wanatibiwa ila sijawahi jua gharama halisi
Angalia pia pad unayosaini huwa ina figure, lakini pia inawezekana wamekosea namba yako ya simu. Siku ukienda waambie wacheki vizuri namba yako
 
Njoeni huku kwenye matibabu ya hukakika kwa gharama ya 261,000 tu
 
siku hizii hata hizo form huzioni... utasign kielectronics baada ya siku kadhaa utaambiwa ulitumia dawa za sh kadhaaa imeishaa hiyo.
 
Ni kweli kabisa, tena si NHIF hata bima zingine pia. Huwa hawafungi mahesabu. Nilimuuliza nesi mmoja mtaani kwa nini inakuaga hivyo alinijibu hivi "...... huko ndiko tunakoponeaga". Hivyo bas, utakuta gharama zako halisi za matibabu ni 30,000 ila hiyo fomu itachezewa iandikwe hata 130,000. Kuna dawa utaambiwa hazipo nenda kanunue nje, ila utakuta umeandikiwa kwenye fomu baadae kua walikupa😳
 
Habari za leo wadau kuna jambo mara nyingi nakutana nalo sijui kama wenzangu hili mmewahi kukutana nalo, kuna hizi form za matibabu NHIF unaenda hospitali unapata huduma kila gharama zinaandikwa kwenye form ukimaliza matibabu unaenda mapokezi kwa ajili ya kuchukua kadi yako ukifika pale inakupasa kusaini ile form ya gharama ulizotumia.

Ila sijawahi kuona ile form hesabu zimefungwa mara nyingi hesabu zinakuwa wazi, hii ni kwanini maana kuna uwezekano ikatokea hospital ambazo sio waaaminifu wakaongeza gharama ambazo hukutumia wewe, sasa sijui shida inakuwa wapi maana tunasaini hesabu ambayo haijakamilika kwanini hii NHIF waingalie kama ndio Sheria wabadili lazima mtu inasaini kitu halisi ulichotumia.
bima ya afya ni kitengo cha uwizi
 
Back
Top Bottom