Kwanini tumekubali ziwa la Kanda ya Ziwa kupewa jina na Malkia Victoria wa Uingereza?

Kwani Ethiopia walitawaliwa na nani ? Mbona wana maendeleo ?
 
Mbona husemi juu ya majina ya kiarabu ?
 
Tena huyu malkia alikuwa anatawala Uingereza miaka ile ya mkutano wa kugawana bara la Afrika.

Kwanini miaka yote hii tangu uhuru hatujarudisha jina lake la asili?

Jina la asili ni lipi hilo mkuu? Maana huku mitaani kuna street names ya ajabu ajabu hata kuyataja unaona aibu kwa mgeni wa kutoka nje
 
Tena huyu malkia alikuwa anatawala Uingereza miaka ile ya mkutano wa kugawana bara la Afrika.

Kwanini miaka yote hii tangu uhuru hatujarudisha jina lake la asili?
Liite ziwa Chato ikikupendeza! Regacy🤣
 
Pekua pekua yangu imeonyesha kuwa ziwa hilo kwa upande wa Tanzania lilifahamika kama "Nyanza Kerewe". Sijui kwa upande wa Kenya(Kisumu) Uganda na Bukoba liliitwa jina gani. Jumuia ya Afrika Mashariki kupitia hawa wabunge wanaochaguliwa sasa, waangalie namna ya kubalilisha hilo jina kama ishara ya uasi kwa Mfalme wa sasa wa Uingereza ambaye amejipambanua wazi wazi kama mbaguzi hasa kwa watu wenye asili ya Afrika.
 
Hata bila wao tungeadvance

Hapajawahi kuwa na jamii domant, umetawaliwa kifikra ukatawalika
 
...Mbona Raisi wa ilivyokuwa Zaire aliweza?? Yeye Mwaka 1973 ama 1974 aliamka asubuhi na kuamuru Raia wake Wote waachane na Majina ya Kizungu na Wote wawe na Majina ya Kiasili.....na yeye Mwenyewe Akaaza na...Mobutu See Seko Kuku Gbendu wa Zabanga?
 
Nina mashaka na race yake
 
Berlin conference ilikuwa mwaka 1884.Alikuwa bado hajazaliwa.Alizaliwa 1926.Sasa,yeye kama Eliza,alimuua babu yako gani?
Hii mada inamzungumzia Victoria ambaye alikuwa malkia na ndio jina lake limepewa ziwa.
 
Hilo ziwa limamilikiwa na nchi 3 sidhani kama Kenya na Uganda watakubali hilo jina unalosema la asili. Yatakuwa yale yale ya ziwa nyasa dunia nzima inaliita Lake Malawi hadi ramani za Google zinaonesha hivyo ila sisi tunaita ziwa nyasa
Ziwa Victoria mbona linaitwa ziwa Nyanza tayari, sema hii Nyanza haijatiliwa tu mkazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…