Kwanini tuna wapinzani wengi mitandaoni ila uraiani hawaonekani?

Ukifuatilia kwa umakini kabisa utabaini kuwa kundi lililopo mtandaoni linatofautiana kwa mbali sana na kundi ambalo kwa sehemu kubwa halingii mtandaoni ambalo ndilo kundi kubwa zaid
 
Nchi hii hakuna upinzani, wale nyumbu wa gaidi wamepoteana siku nyingi.
 

Nyani wale wale pori jipya:

 
Walio mtandaoni wana accsess ya habari na wanajua yanayotokea. Watu wengi hawana hiyo na wengi wako vijijini.
Mazingira ya siasa si rafiki wengine humu ni watumishi

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hizi ndio hoja za UVCCM poor mind

Sasa unataka kusema kuwa hao wapinzani wa mitandaoni wanaishi wapi...jiulize! Wanaishi dunia ingine

Ccm ruhusuni mikutano ya siasa, na maandamano ya amani, hao wapinzani mtawaona tu

Police ndio mbeleko ya CCM...unajitoa ufahamu tu

Kama hakuna wapinzani, Mbona mnawatumia police
 
Jamhuri ya mitandao
 
MMh haya bwana
 
umedanganyika sana , yaani ulivyo na akili duni unadhani Polisi watawasaidieni hadi lini ? Aliyempindua dikteta Alfa Conde alikuwa mshika mwamvuli wake akihutubia juani au kwenye mvua
Yaani ktk punguani ninaonza kuwaona jf wewe unaweza shika namba moja.

Hapa tunazungumzia wapinzani au jeshi?.

Si lazima kujadili jambo kama bado hujapevuka kuchambua na kuelewa, hebu tafuta mada inayohusu Guinea kuna andiko langu humo alafu rudi nikupe elimu!.
 
Nchi hii kuna wapinzani basi,wote ni wachumia tumbo au wananufaika na mfumo husika ndio maana hawawezi kujitokeza hadharani wanajificha mitandaoni.
 
Wanasema wanamtegemea Mungu, Mungu atawalipia! Cowards kabisa hawa jamaa! Ila ukiwakuta nyuma ya keyboard unaweza dhani ni akina Che Guavara
Na jambo baya kabisa kuna vijana hapa jf wanaanza kuliona jeshi la Guinea eti limewasaidia upinzani kupindua nchi, yaani hawa keyboard warriors wanamambo ya ajabu sana!.
 
Mimi bado nadhani ni wachache sana, na serikali ina fanya vyote ulivyovitaja ili wasije wakawa wengi! Maana upotoshaji unao tumika, serikali isipo wacheck, wanaweza kuongezeka! Ni hilo tu, ila wapinzani ni wachache sana.
 


Labda mtaani kwako unakoishi ndio hawapo. Mtaani kwangu wapo wengi sana

Lakini pia hoja yako haina mashiko. Ni hoja mfu katika uwanja wa taaluma ya siasa au labda umeamua tu kujitoa ufahamu
 
Ukitaka kuwaona wapo, basi Shughuli za kisiasa za vyama zisizuiliwe as if ni vita au uhaini, utawaona wananchi wakihudhuria mikutano, makongamano kwa wingi sana! etc
 
Mleta mada labda uelewi Chadema inaenda na utandawazi wewe uko wapi, au uelewi maana ya Chadema DIGITALI. Maana ya digitali ni kinyume cha ANALOGI sasa unataka kuturudisha nyuma. Chadema ni vinanda mpaka kieleweke.
 
Usiku wa kuamkia maandamano sikulala vizuri, milio ya magari a polisi yalikesha. Kesho yake barabara mjini kwetu zilijaa migambo na raia wa kawaida waliogopa kwenda hata sokoni.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Ndo ujue wa kuutoa uhai kwa ajili ya wengine hayupo.
Lissu si angeingia barabarani kuonyesha mfano?
 
Waulize wazambia wametumia mitandao kumuondoa lungu
 
Na jambo baya kabisa kuna vijana hapa jf wanaanza kuliona jeshi la Guinea eti limewasaidia upinzani kupindua nchi, yaani hawa keyboard warriors wanamambo ya ajabu sana!.
Ni wa kutandika hawa jamaa, halafu wanajiona special sana! Mkutano na Samia hawataki kwenda na vyama vingine, wanataka waende peke yao!! Kila siku wanasumbuana na polisi, wanalalamika kila siku, Msajili wa vyama anawaambia anaandaa mkutano na Polisi ili kila upande useme tatizo ni nini, yanayowezekana yatatuliwe, wao wanakataa, wanasema Msajili anavunja katiba, wao hawawezi kushiriki kuvunja katiba!!Unafiki mkubwa, chama chao kikomo cha Mkiti ni miaka 10, Mbowe kavunja katiba anatoboa miaka 20 sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…