Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

ndugu yangu wasukuma watakukoma mwaka huu
Wasukuma bwana wana shida na ndio wanao facilitate hii kampeni ya kumu undermine mama kwasababu tu mtu wao aliye waaminisha kuwa yeye ni jiwe
 
Mbona tayari imetokea?
 
Hivi nyie watu huwa hamsomi katiba au ni ujuaji kutoka vichwani mwenu

Kikatiba samia ni rais kamili na hii ni awamu yake ya sita na ananafasi moja ya miaka mitano kugombea tena full stop
 
Kama mama anahudumu awamu ya 5, basi atakaa madarakani kwa Muda wa miaka 14, ni rahisi tu ikifika 2030 achukue fomu ya urais na ajenge hoja kuwa 2021 hadi 2025 alikuwa anahudumu miaka ya magufuli, na 2025/2030 ndo awamu yake ya kwanza na ya pili atamalizia 2030/2035. Simple like that.
 
Ukijua maana na matumizi ya neno awamu hili halitokusumbua...
Lakini kisaikolojia naona anajitahidi sana kuiaminisha dunia kuwa tutegemee utawala wake utachukua mrengo wa tofauti ukilinganisha na mtangulizi wake...
Hili ni muhimu na ndo linamfanya aone yeye ni wa awamu ya 6!

NB: ccm imeparaganyika sana. Upinzani wanazidi kutuchelewesha!
 
Soma katiba vizuri....
raisi atakapotoka madarakani kwa sababu yyte ile......kabla ya muda wake kuisha.....makamu atamalizia kipindi kilichobaki....
 
Hapo nafikiri aujaelewa,hebu fikiria kama membe angechukua fomu na magufuli kutokupitishwa alafu membe awe rais ingekuwa ni hawamu ya tano tena?.
Mwinyi, Mkapa, JK wote walikula vipindi viwili viwili so kwa ni i awamu zao mmeunganisha kuwa mojamoja na leo mnasema awamu ya 5/6, kwa nini msiseme awamu ya 10 au 11..?
 
AWAMU ZINAHESABIWA KWA MABADILIKO YA RAIS . SI LAZIMA RAIS APATE MIHULA MIWILI KWA KUWA UCHAGUZI HUFANYWA KILA MIAKA MITANO NA KITI CHA RAIS KINAWEZA KUCHUKULIWA NA CHAMA CHOCHOTE KILICHOSHIRIKI.
 
Yani mtoto wa darasa la 7 akiulizwa Rais wa awamu ya tano ni
A.Magufuli
B.Samia
Atajibu nini ?

Awamu ya uongozi ni mtu na vipindi vyake.
Mama Samia kaapa kuwa Rais ,ni katiba iko hivo.
Lazima awamu yake iitwe hivo.
Mwendazake kafa na awamu yake ya 5.
 
Kwamba ni serikali ya Rais wa sita na sio awamu ya sita. Kwamba awamu ingehusisha uteuzi wa waziri mkuu na mwanasheria mkuu. Mama SSH ni Rais wa sita anaekamilisha awamu ya tano(maelezo ya wanasheria)
 
Kwamba ni serikali ya Rais wa sita na sio awamu ya sita. Kwamba awamu ingehusisha uteuzi wa waziri mkuu na mwanasheria mkuu. Mama SSH ni Rais wa sita anaekamilisha awamu ya tano(maelezo ya wanasheria)
Kwa hiyo Rais akichagua waziri mkuu mwingine awamu ndio itakuwa imebadirika?
 
Generalist njoo startv Kuna majibu
Nimeona na Kusikia pia Ndugu. Nashukuru kile nilichojifunza na Kujiamini nacho kwa 100% ndicho Kimesemwa na huyo Lawyer hapo Studioni Stsr Tv.

Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita katika Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )


Ninashangaa kuliona hili halijaeleweka.
 
Na kwamba viapo vya mawaziri havija expire
Kinachobadilisha awamu ni Kiongozi Mkuu wa Nchi na sivinginevyo wapo baadhi ya mawaziri walikuwepo toka kipindi cha Nyerere mpaka sasa lakini uwepo wao haukuzuia awamu kubadilika

Hata mama ni kwa sababu ya joto la kisiasa tu lakini huyu pm tulie nae muda si mrefu atambadilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…