Kwanini tunapenda kushabikia vita?

Kwanini tunapenda kushabikia vita?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Mimi siwaelewi watu wanaoshabikia vita kama vile ni Premier League. Hivi hatuelewi huko Ukraine, Gaza na sasa Lebanon watu (ikiwa pamoja na watoto) wanakufa, wanapata ulemavu na maisha yao kuharibiwa kwa kosa ambalo sio lao?

Unahisi kabisa excitement ya watu wanapozungumzia mabomu yanavyoangushwa, nyumba zinavyolipuliwa na wanajeshi wanavyovamia!

Kwa kweli inasikitisha.

Amandla!
 
"Muvi" zimewaharibu toka wakiwa wadogo!

Wazazi mnalo la kulaumiwa hapa.. watoto wanashinda mabanda ya Video baadaye wanakuwa watu wazima wa hovyo! Kazi unazi wa mpira na vita!
 
Dunia imejaa wapumbavu wengi wanaojona wao ndio wenye hakimiliki na dhamana ya kuishi, wanaua na kuteswa wenzao sasa watu kama hawa hawastahili kuendelea kuwepo kwenye ulimwengu wa waliostaarabika kwahiyo wakipigwa kama una akili timamu unaunga mkono tu .
 
nato allies nyuma ya israel....tz tupo nyuma ya hizbulaa
FB_IMG_1697199849150_1.jpg
 
Ungeanza kuwashangaa kwanza watu wazima wanaobeba silaha na kuanza kuuana. Nadhani binadamu hatuna akili za kutosha kutuwezesha kuishi kwa amani. Ukosefu huo huo wa akili ndiyo unatufanya tushangilie na vita.
 
Mimi siwaelewi watu wanaoshabikia vita kama vile ni Premier League. Hivi hatuelewi huko Ukraine, Gaza na sasa Lebanon watu (ikiwa pamoja na watoto) wanakufa, wanapata ulemavu na maisha yao kuharibiwa kwa kosa ambalo sio lao?

Unahisi kabisa excitement ya watu wanapozungumzia mabomu yanavyoangushwa, nyumba zinavyolipuliwa na wanajeshi wanavyovamia!

Kwa kweli inasikitisha.

Amandla!
Unapoteza muda kuwashangaa wanaoshabikia vita badala ya kuwashangaa wanaopigana hiyo vita. Mtu mzima kushika bunduki na mabomu kuwinda uhai wa binadamu mwenzio ni zaidi ya upunguani.
 
Usiseme wapenda vita, sema wanaharakati wa mitandaoni... Wapo wengi na kila mmoja anaamini katika anachokiamini juu ya mienendo ya mataifa flani duniani..

Mara nyingi wachangiaji hawa wa mada za vita utawakuta pia kwenye mijadala ya kisiasa ya dunia, uchumi, technology n.k.. na hawa huwa sio vilaza , wengi wanajielewa..

Halafu fahamu kitu kimoja, hii dunia toka enzi zimekuwepo vita, ukisoma biblia utakuta kuna hadithi za vita, quran vile vile...

Huko kanisani mbona wanafundishwa Daudi alimuua Goliath akamkata kichwa halafu mnashangilia kwa amina nyingi? Na mchungaji anafurahia mauaji? Waumini wanafurahia mauaji?

Kuna faida za vita, kama Hitler kudhibitiwa WW2 na dunia ikawa mahala salama, kuna ambao walikuwa na mitizamo Hitler was right wengine wakaona ni gaidi.. hivyo lazima hizo pande watofautiane kuanzia mtaani hadi mitandaoni...
 
Unapoteza muda kuwashangaa wanaoshabikia vita badala ya kuwashangaa wanaopigana hiyo vita. Mtu mzima kushika bunduki na mabomu kuwinda uhai wa binadamu mwenzio ni zaidi ya upunguani.
Umewaza kama mimi kwa 💯%.

Wanaopigana vita ndo wa kuwashangaa.

Na cha kushangaza zaidi, eti kuna hadi sheria za vita.

Yaani kuna mambo yanayokubalika na yasiyokubalika.

Kwa akili yangu, vita ndo inayopaswa kutokukubalika.

Lakini ndo hivyo tena.

Kwa hiyo uko sahihi kabisa. Wanaobeba silaha na kuanza kuuana ndo wanawajibika moja kwa moja kwa kila kinachotokea vitani na ndo wanaopaswa kushangaliwa.
 
Kabisa100%
 
Unapoteza muda kuwashangaa wanaoshabikia vita badala ya kuwashangaa wanaopigana hiyo vita. Mtu mzima kushika bunduki na mabomu kuwinda uhai wa binadamu mwenzio ni zaidi ya upunguani.
😁😁😁
 
Mimi siwaelewi watu wanaoshabikia vita kama vile ni Premier League. Hivi hatuelewi huko Ukraine, Gaza na sasa Lebanon watu (ikiwa pamoja na watoto) wanakufa, wanapata ulemavu na maisha yao kuharibiwa kwa kosa ambalo sio lao?

Unahisi kabisa excitement ya watu wanapozungumzia mabomu yanavyoangushwa, nyumba zinavyolipuliwa na wanajeshi wanavyovamia!

Kwa kweli inasikitisha.

Amandla!
Breaking: Israel imemuua Hassan Khalil Yassin, aliyechukua nafasi ya Hassan Nasrallah masaa machache yaliyopita.

Hii inavunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa muda mfupi zaidi kama mkuu wa shirika la kigaidi.

Yaaan Hassan baada ya kuuwawa basi wakateua bwana Hassan Yasin kushika nafasi naye hakumaliza masaa

Netanyahu kaiambia dunia kwamba mkono wa israel hakuna sehemu hauwezi fika dunian
 
Mimi siwaelewi watu wanaoshabikia vita kama vile ni Premier League. Hivi hatuelewi huko Ukraine, Gaza na sasa Lebanon watu (ikiwa pamoja na watoto) wanakufa, wanapata ulemavu na maisha yao kuharibiwa kwa kosa ambalo sio lao?

Unahisi kabisa excitement ya watu wanapozungumzia mabomu yanavyoangushwa, nyumba zinavyolipuliwa na wanajeshi wanavyovamia!

Kwa kweli inasikitisha.

Amandla!
Sisi wa machinga wauza dawa za mende,kubuni ,viroboto na chawa vita za huko Gaza zinatuhusu nini mkuu.
Ukrain kwao ni vita inayopoteza watu wao kwa Tamaa za watawala na harakati za kijinga za binadamu kisiasa na kidini.

Hapa kwetu tunaona pia watu wanauana sana . Lakini serikali haijali sana kwa sababu wanaangalia siasa na dini .

Padri akimwagiwa tindikali Waislam wanaona poa tu .
Chadema wakitekwa na watu wasiojulikana CCM na polisi wanasema achana nao wamalizwe tu wanajiteka na kujipiga risasi wenyewe.
Yaani mtu akipiga risasi 17 mwenyewe kisha anaachwa kushitakiwa kwa kujaribu kujiua ili kukomesha hiyo tabia ya kujipiga risasi .
Mtu anajitoka na kujipiga na kujijeruhi karibu kufa lakini hakamatwi na kufikishwa mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo na kuleta taharuki lakini anayesema kuwa ndugu yetu amepotea ndiye anayekamatwa. Mtu anajiteka badala ya kuchukuliwa hatua kali unaona yupo na viongozi wa CCM au Polisi amezungukwa na vyombo vya habari kama shujaa . Mkuu wa nchi haoni huo upuuzi na kuukemea anasema wanatekana kwa sababu wanapenda tabu.
Padri akiikosoa serikali wanasiasa wanakuja juu eti wanachanganya dini na siasa.
Ustaadhi akitekwa anayepiga kelele ni Shekhe Ponda peke yake.
Viongozi wa CCM wakiuawa kama kule Kibiti Oparation kali inafanyika kwa sababu inaonekana ni Ugaidi.

Huu upuuzi wa kukiuka haki kwa sababu ya sasa na dini ndio chanzo cha vita duniani.

Sasa ushabiki wa vita unategemea yale yale yanayofanyika ndani ya nchi zote kushabikia siasa za watawala au dini za wananchi.

Lakini pia Wazungu na waarabu na wachina walishatuzoesha kupenda Move za vita .
Kwa hiyo tukiona wanalipua bomu basi hatuamini kuwa ni kweli tunaamini kuwa ni move tu za Rambo. 😂😂😂😂
Move ya Ukrain na Staring wa move ni Putin inanoga lilipigwa bomu na kugeuza ardhi juu chini.

Yote haya chanzo ni watu wema walikaa kimya au walijitenga na siasa na kuwaacha watu waovu na mashetani watawale dunia nzima .
Dunia haiwezi kuwa na amani tena kwa sababu wale waovu ndio wanaounda UN na wanakutana kujiwekea taratibu za kulindana wao na sio kizazi cha wanadamu wote ukizingatia wengi wao wana mtoto mmoja au hawana kabisa na wengine ni mashoga na wasagaji.

Dunia ni uwanja wa vita kati ya wema na uovu.
Kuna timu wema(Mungu au Haki) na timu uovu(Shetani au dhulma )

"'"Duniaaaaa" Vita iendelee ."
 
Back
Top Bottom