Mimi siwaelewi watu wanaoshabikia vita kama vile ni Premier League. Hivi hatuelewi huko Ukraine, Gaza na sasa Lebanon watu (ikiwa pamoja na watoto) wanakufa, wanapata ulemavu na maisha yao kuharibiwa kwa kosa ambalo sio lao?
Unahisi kabisa excitement ya watu wanapozungumzia mabomu yanavyoangushwa, nyumba zinavyolipuliwa na wanajeshi wanavyovamia!
Kwa kweli inasikitisha.
Amandla!
Sisi wa machinga wauza dawa za mende,kubuni ,viroboto na chawa vita za huko Gaza zinatuhusu nini mkuu.
Ukrain kwao ni vita inayopoteza watu wao kwa Tamaa za watawala na harakati za kijinga za binadamu kisiasa na kidini.
Hapa kwetu tunaona pia watu wanauana sana . Lakini serikali haijali sana kwa sababu wanaangalia siasa na dini .
Padri akimwagiwa tindikali Waislam wanaona poa tu .
Chadema wakitekwa na watu wasiojulikana CCM na polisi wanasema achana nao wamalizwe tu wanajiteka na kujipiga risasi wenyewe.
Yaani mtu akipiga risasi 17 mwenyewe kisha anaachwa kushitakiwa kwa kujaribu kujiua ili kukomesha hiyo tabia ya kujipiga risasi .
Mtu anajitoka na kujipiga na kujijeruhi karibu kufa lakini hakamatwi na kufikishwa mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo na kuleta taharuki lakini anayesema kuwa ndugu yetu amepotea ndiye anayekamatwa. Mtu anajiteka badala ya kuchukuliwa hatua kali unaona yupo na viongozi wa CCM au Polisi amezungukwa na vyombo vya habari kama shujaa . Mkuu wa nchi haoni huo upuuzi na kuukemea anasema wanatekana kwa sababu wanapenda tabu.
Padri akiikosoa serikali wanasiasa wanakuja juu eti wanachanganya dini na siasa.
Ustaadhi akitekwa anayepiga kelele ni Shekhe Ponda peke yake.
Viongozi wa CCM wakiuawa kama kule Kibiti Oparation kali inafanyika kwa sababu inaonekana ni Ugaidi.
Huu upuuzi wa kukiuka haki kwa sababu ya sasa na dini ndio chanzo cha vita duniani.
Sasa ushabiki wa vita unategemea yale yale yanayofanyika ndani ya nchi zote kushabikia siasa za watawala au dini za wananchi.
Lakini pia Wazungu na waarabu na wachina walishatuzoesha kupenda Move za vita .
Kwa hiyo tukiona wanalipua bomu basi hatuamini kuwa ni kweli tunaamini kuwa ni move tu za Rambo. 😂😂😂😂
Move ya Ukrain na Staring wa move ni Putin inanoga lilipigwa bomu na kugeuza ardhi juu chini.
Yote haya chanzo ni watu wema walikaa kimya au walijitenga na siasa na kuwaacha watu waovu na mashetani watawale dunia nzima .
Dunia haiwezi kuwa na amani tena kwa sababu wale waovu ndio wanaounda UN na wanakutana kujiwekea taratibu za kulindana wao na sio kizazi cha wanadamu wote ukizingatia wengi wao wana mtoto mmoja au hawana kabisa na wengine ni mashoga na wasagaji.
Dunia ni uwanja wa vita kati ya wema na uovu.
Kuna timu wema(Mungu au Haki) na timu uovu(Shetani au dhulma )
"'"Duniaaaaa" Vita iendelee ."