Naomba uiangalie CCM kwa karibu zaidi; na baada ya kufanya hivyo, bila ya kujipindisha akili, uje tena hapa ueleze jinsi "mfumo" unao uabudu huko unavyo fanya kazi.mnafanya kosa kubwa sana kuabudu watu badala ya kujenga taasisi, mwisho wa tundu lisu au mbowe haupaswi kuwa mwisho wa chadema kama chama, chama siyo mtu mmoja or haipaswi kuwa hivyo atleast, chadema inapaswa iwepo long after hata hao akina tundu lisu na mbowe wasipokuwepo.
kwa maoni yangu mnawekeza sana matumaini na mategemeo kwa binadamu ambao siajabu kiuhalisia hata hamuwajui vizuri matokeo yake ndiyo disappointments kila siku, mtegemeeni Mungu na siyo sijui tundu lisu au mbowe kwa maana wote ni binadamu wenye mapungufu …
Hiyo "taasisi" inayo ishikiria CCM unaiona?
Sasa utueleze jinsi gani CHADEMA inavyo weza kuinyakuwa taasisi hiyo hiyo.
Mimi nitakwambia bila ya kupepesa macho, wala kutikisa masikio, kwamba taasisi pekee yenye maana ni ya umma wa waTanzania, basi. Hakuna taasisi nyingine zaidi ya hapo.
Nawasihi sana CHADEMA, watakapo maliza kukisafisha chama chao na kuondoa hizi takataka za akina Mbowe, kazi yao kubwa iwe ni kuijenga hii taasisi muhimu na kuipa imani juu yao. Wananchi ni muhimu wakiamini hiki chama kuleta mabadiliko katika maisha yao.