Kwanini tunatafsiri mshale wa saa kinyume na inavyoandikwa - hii inatokana na nini?

2013

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
11,360
Reaction score
6,069
wana JF ningeomba hapa mnijuze wale mnaoelewa hilijambo kwa undani zaidi manake najiuliza sijui ni utumwa ama nini?, manake siielewi hii, kukuta saa inaandikwa nane(8) lakini inasomwa mbili(2), ama inaandikwa kumi(10) lakini inasomwa nne(4). huu utaratibu wa kusoma saa ndivyo sivyo ulitokana na nini?.

pia je na wazungu (waingereza) ama hata wamarekani huko makwao wanasoma hivyohivyo mishale ya saa?. ama wanafuata mtindo huo wa namba.ningeombwa wenye kuelewa chanzo mtujuze.

Masaa unayoyahesabu wewe ni ya kiarabu vile wao huanza siku saa 12 asubuhi. Watu wa magharibi siku huanza baada ya saa 6 usiku na ndio utaratibu duniani kote. Pia kiarabu wiki huanzia jumamosi wakati wamagharibi siku huanza jumatatu.
 
...hii kitu Lawino ilikuwa inamchanganya sana. Ref "song of lawino" anasema vi2 vinakwenda up side down. Ikiwa 1 anaambiwa saa 7, wakati yeye alikuwa akiangalia jua tu anajua saa ngapi! Hapa kuna hoja.
 
Sina uhakika but kuchangia sio ujinga either, i heard that somehow inahusiana na freemason kuhusu no 6
mfano 7-1=6
8-2=6
9-3=6
10-4=6 na kuendelea

kwenda na conclusion kama hio ni ujinga cc Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Sina uhakika but kuchangia sio ujinga either, i heard that somehow inahusiana na freemason kuhusu no 6
mfano 7-1=6
8-2=6
9-3=6
10-4=6 na kuendelea

Hata mimi nilisikia hivyo.
Yani ukichukua zile namba ukitoa namba za saa halisi unapata common difference ambayo ni 6
 
Masaa unayoyahesabu wewe ni ya kiarabu vile wao huanza siku saa 12 asubuhi. Watu wa magharibi siku huanza baada ya saa 6 usiku na ndio utaratibu duniani kote. Pia kiarabu wiki huanzia jumamosi wakati wamagharibi siku huanza jumatatu.
Ila Mkuu, sio kweli Duniani kote week huanzia J/3. Portugal week huanzia Domingo sawa na J/pili.
 
kwenda na conclusion kama hio ni ujinga cc Kiranga

Mkuu tuambie basi huo ujanja kama wenzio wanachangia halafu unaita ujinga

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Is a conventional way of communicating. Kumbuka lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalum na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano. Kama wanadamu, tumekubaliana iwe hivyo na tunaelewa kinachoonekana.
 
Masaa unayoyahesabu wewe ni ya kiarabu vile wao huanza siku saa 12 asubuhi. Watu wa magharibi siku huanza baada ya saa 6 usiku na ndio utaratibu duniani kote. Pia kiarabu wiki huanzia jumamosi wakati wamagharibi siku huanza jumatatu.

Hapa hata mimi umenifumbuwa macho.
 
Hata wazungu flani wa sauz walishaniuliza hilo swali.
 
Siku kwa mujibu wa mfumo wa kimagharibi inaanza saa sita za usiku, wich is weird.

Katika mfumo wa Kiswahili siku inaanza saa moja asubuhi.

Tatizo tunachanganya mifumo, tunatumia mfumo wa kimagharibi ambao siku inaanza saa sita usiku lakini tukisoma kiswahili tuna soma saa kwa mfumo unaofuatisha siku inayoanza saa moja asubuhi.

Saa ya Kiswahili inatakiwa kuonesha saa moja pale ilipo 1. Nishawahi kuona saa iliyokuwa set hivyo.

Sadly, aliyefanya hivyo ni mzungu aliyependa Uswahili.
 
Ila Mkuu, sio kweli Duniani kote week huanzia J/3. Portugal week huanzia Domingo sawa na J/pili.

Sina hakika na huko Portugal ila najua hili:

Sina uhakika but kuchangia sio ujinga either, i heard that somehow inahusiana na freemason kuhusu no 6
mfano 7-1=6
8-2=6
9-3=6
10-4=6 na kuendelea

Mwenye thina uhakika but kuuliza si ujinga!
Hizo hesabu ulizoziweka mbona ukiikusudia nö yoyote inakuja hivyo hivyo?
mfano, nö 4
5-1=4
6-2=4
7-3=4
8-4=4 na kuendelea....
...
Au mimi thijaelewa!
Embu alieelewa hasabu za jamaa na mahusiano yake ktk mpangilio wa usomwaji saa.
 
Masaa unayoyahesabu wewe ni ya kiarabu vile wao huanza siku saa 12 asubuhi. Watu wa magharibi siku huanza baada ya saa 6 usiku na ndio utaratibu duniani kote. Pia kiarabu wiki huanzia jumamosi wakati wamagharibi siku huanza jumatatu.

Kwa uwelewa wangu nahisi hapo underline ndio jibu la mleta mada!
...
kuhusu kutumika duniani kote sidhani, coz waarabu (especialy islamic states) ni wagumu kweli kufuata kila kitu kilicholetwa na wazungu, zaidi hiko kitu kiende against na imani ya dini yao! Mwenyewe si unaona sheria zao za barabarani na magari yao, ie dereva anatakiwa apite kulia instead of kushoto, na gari zao skani ziko upande wa kushoto!
Sasa hapa kwenye issue ya kusoma saa, ukizingatia wana saa zao according to imani yao, na vile vile wanaviwanda vyao vya kutengeneza saa! Mmmh! Sidhani kama wanasoma saa kama wazungu!
 
I have a question, kama hapa Tz(ingawa haifuatwi na wengi) siku huisha saa moja jioni(jua linapozama) na siku huanza saa moja asubuhi(jua linapochomoza), huu muda kati ya saa moja ya jioni na saa moja asubuhi inakuwa ni siku gani hasa? Na tarehe yake ni ya siku iliyoisha au inayofuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…