Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
Siku kwa mujibu wa mfumo wa kimagharibi inaanza saa sita za usiku, wich is weird.
Katika mfumo wa Kiswahili siku inaanza saa moja asubuhi.
Tatizo tunachanganya mifumo, tunatumia mfumo wa kimagharibi ambao siku inaanza saa sita usiku lakini tukisoma kiswahili tuna soma saa kwa mfumo unaofuatisha siku inayoanza saa moja asubuhi.
Saa ya Kiswahili inatakiwa kuonesha saa moja pale ilipo 1. Nishawahi kuona saa iliyokuwa set hivyo.
Sadly, aliyefanya hivyo ni mzungu aliyependa Uswahili.
Na mimi kamwe huwezi kuta saa yangu nimeset kizungu.
Mwenyewe nishazoea fresh. Coz hakuna logic ya kuset masaa yetu kizungu wakati kiuhalisia tupo kinyume na mzunguko wao wa masaa na kuanza kwao kwa siku.