2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,360
- 6,069
- Thread starter
- #61
ha ha ha haha, nimeipenda hii. nimekuelewa mkuu. duh!!:smile-big:mimi mtu yeyote atakuwa sahihi pale ambapo saa itakuwa imeandikwa saa (8) yeye akasema ni saa (2). Kwa nini nasema hivyo?
Hii inatokana na sababu kuwa ni saa (8) tokea siku mpya ikiwa imeanza yaani baada ya saa (6) mchana au usiku.
Na atakaye sema saa (2) yuko sawa kwa sababu ni saa (2) baada ya jua kuchomoza au kuzama.
Kwa maana hiyo basi unakuta saa inasema saa (8) asubuhi. Sisi tunatafsiri kuwa ni saa (2) asubuhi, tukiwa na maana kuwa ni masaa (2) tokea jua lichomoze.
Vivyo hivyo ukikuta kwenye saa imeandikwa saa (8) usiku. Mtu akikuambia ni saa (2) usiku yupo sawa kwa sababu anamaanisha ni masaa (2) tokea jua lizame.
Naamini nimeeleweka.