Kwanini tusijenge Bandari ya Bagamoyo tusijenge kwa fedha zetu wenyewe?

Kwanini tusijenge Bandari ya Bagamoyo tusijenge kwa fedha zetu wenyewe?

Ndege zinafaida mtambuka ambazo CAG hazikagui. Tujenge kwa fedha zetu khalafu waliobuni huo mradi wale vipi.

Ni wazo zuri inaweza kujengwa hatua kwa hatua. Hatua ya kwanza unajenga mpaka ianze kuoparate kwa uhitaji wa sasa. Hatua nyengine zitaendelezwa kwa faida itokanayo na hatua ya kwanza na mahitaji yakiongezeka.

..faida mtambuka za atcl ni zipi?

..Je, mashirika binafsi ya ndege hayawezi kutupatia faida mtambuka zinazoletwa na atcl.
 
Maendeleo ya kijamii- ajira mtambuka kuanzia kwa walima korosho zinazogawiwa ndani ya ndege. Maendeleo ya kiuchumi ikiwemo kuharakisha baadhi ya utendaji. Mfano ni mwili wa mwendazake kuagwa kwake kulivyo rahisishwa na kufanikisha wengi kuhusishwa.

Mashirika binafsi hayawezi kuwa alama ya Taifa/nchi,ATCL ni kama bendera ya Taifa.
 
Kaka point ni watanzania na serikali yetu iwe na share zaidi ya 50% or kiasi kwa ujumla ndani ya hiyo Bandari.
Na kumbuka kama hizi estimation na mchoro wameleta Wachina. Wanaweza kuwa wame over estimated kaka.
Anyway mawazo yangu tuu. Kulika kuwapa 100%.
They didn't over estimate, hiyo ni investment na walikuwa wanakopa hela kutoka Oman, and why waoverestimate since hawapewi hela bure????? Simple logic tu.
 
Unamaana gan Daniel.? Sijakupata.
Msomi anarise hoja kwa kukupa facts Kama ulizozitoa wewe na wasomi wenzie wenzie wanambishia kwa kumpa facts zingine wanazozijua kitaalamu. Darasa la Saba wanakulazimisha tu uamini mawazo ya mtu Fulani bila kukupa upembuzi yakinifu kuhusu msimamo huo. Pia darasa lasaba wanakujibu hoja moja wakati wewe umetoa hoja kumi na wanakuhukumu kwa hoja moja Kati ya kumi ulizotoa.
 
Hili linawezekana Mkuu, ni Ubunifu tu.
Changamoto ni pale inapotokea mifuko yetu inapopungua, vyuma vinapokaza. Je, tutakuwa tayari? Au tutasaliti Matamanio yetu kwa kutojua gharama sake?
Lakini pia vipo vibano vya nje, usishangae ukawa unajenga yako Bagamoyo, mchina akaweka yake Lamu au Pemba ya Msumbiji.

Safari yetu ni ndefu na ngumu mno.
Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu.
 
Wazo zuri mno ndugu yangu rodgers123. Naomba nikiri kwamba binafsi niliwahi kuliwaza hili siku za karibuni nikiwa napitia mfumo wa uwekezaji wa mafuta uliopo kule chini Norway. Kama Mungu akinipa Neema nadhani ntaandika Paper kuhusu hili,......

TURUDI KWENYE MADA: Ni vema sana kupata uwekezaji kutoka nje lakini nadhani kuchangia kiasi fulani cha pesa kunasaidia kukupa nguvu na uhuru kimaamuzi na wewe. Binafsi nadhani badala ya kununua ndege na vitu vingine tungejikita kupeleka rasilimali kwenye uwekzaji wa kimkakati kama bandari ya Bagamoyo na gesi ya Mtwara.

Faida kubwa za kiuchumi ambazo tungezipata kutokana na bandari na gesi zingetusaidia sisi Tanzania kufufua ATCL kiurahisi, tungenunua hata ndege mia kwa bei taslimu. Tungepeleka watoto wetu shule bure kabisa, tungekuwa na nguvu kubwa kidiplomasia ukanda huu wote, tungetengeneza maelfu ya ajira na mengineyo mengi tu. Lakini ndiyo hivyo........

NAUNGA MKONO HOJA KWA ASILIMIA 100%,....
 
..faida mtambuka za atcl ni zipi?

..Je, mashirika binafsi ya ndege hayawezi kutupatia faida mtambuka zinazoletwa na atcl.
Shirika la serikali hawezi kupandisha bei ya huduma kizembe, shirika binafsi hawawezi kubeba nembo ya taifa kuonyesha ufahari wa nchi, shirika binafsi wakipata hasara mara moja haooo wanaondoka zao, nk,nk
 
Tatizo la bandari ya Bagamoyo sio pesa au muundo wa ushirikiano.

Hiyo bandari ingekuwa inajengwa Kilwa ingeshajengwa.
 
Mfano hivi kweli tumeshindwa chimba wenyewe Hellium na kuuza wenyewe.
Soma hii document toka Hellium One Company.
Capital yake ya uwekezaji hivi tumeshindwa raise pesa na kuita wataalamu waje wajenge na tuwalipe..?
Mtazamo wangu tuu.
Hii pesa hata bank ya wanawake ingeweza kuwakopesha na sio kuanza kutudhalilisha huko duniani, mama saa100 awaite awaambie hizo hisa wanazotapanya serikali itazinunua
 
Shirika la serikali hawezi kupandisha bei ya huduma kizembe, shirika binafsi hawawezi kubeba nembo ya taifa kuonyesha ufahari wa nchi, shirika binafsi wakipata hasara mara moja haooo wanaondoka zao, nk,nk

..tuliweza kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii bila kuwa na shirika letu la ndege.

..zaidi, mapato yetu yatokanayo na utalii ni makubwa kuliko majirani / washindani wetu, kwa mfano Kny na Rwn, ambao wana mashirika ya ndege ya serikali.

..Kwa maoni yangu hatuhitaji kubeba mzigo wa hasara kwa kuwa na shirika la ndege la serikali. Uko ushahidi kwamba tunaweza kukuza utalii, na kuvutia wawekezaji, bila serikali kumiliki shirika la ndege.
 
Back
Top Bottom