Kwanini Uber haziruhusiwi kuchukua abiria Mwalimu Julius Nyerere International Airport?

Kwanini Uber haziruhusiwi kuchukua abiria Mwalimu Julius Nyerere International Airport?

Kwa Marekani uber/lyft nao wametengewa maeneo yao ya kuegesha na pia sehemu ya kupakia wateja katika viwanja vya ndege, kama ilivyo kwa taxi za kawaida.
Uzuri wao huduma zipo za uhakika na wametengenezewa sehemu
Ingawa wanalipa
Airport Authority ya Tz wangetengeneza hela nzuri kama wanajua kula na kipofu
 
UBBER ZINWVIBAOO VYARANGI YA BIASHARA...RAHISIIKUJUAA..HAPAASHIDAA ZILETAX ZAWAH PALENDANI KYRUHUSU N KULAZAWATOTO NA CHOOKILAINI EBO..JIPANGENI
Dah mpwa leo nimeshindwa kabisa kukuelewa hapa, huwa najitahidi sana nikisoma text zako between the lines nakuelewa ila leo naona nimetoka kapa embu andika tena.
 
Kuna tetesi kwamba zile taxi pale airport ni za wafanyakazi wa pale pale airport.

Lakini pia, kijiwe kama kile kuna wazee wa siku nyingi ambao wanaumoja wao, Na hata wanaweza kukuroga kama ukitaka kuingia kwenye himaya yao. Hawajui sehemu nyingine zaidi ya pale.

La mwisho nadhani pia katika sehemu ambayo inaweza kuharibu taswira ya nchi kwa wageni kuibiwa ni airport. Wageni wengi wanashauriwa wachukue only registered taxi. Na kweli karibia taxi drivers wote pale airport ni waaminifu kwa sababu hapo ndipo ofisi ilipo.
 
Siku Nyingine Niachie Mimi Gari,ntakuja Kukupokea
Mi nikishuka zangu natoka nje Puma pale nakula bodaboda hadi nilikopaki gari fresh,niliwahi kupaki gari mle ndani kwa wiki moja niliimba alelele…bado kuna ujinga kwamba aliepanda ndege ana hela sana,dhana potofu na ya kipumbafu
 
Sina hakika na hilo, leo nimetoka airport na Uber kwenda town.... Ukitaka no. ya gari nakupa. Labda km aliingia kwa kujificha........ But the ride was ok!
siku ukijapata usumbufu utatuletea mrejesho..mana mm madereva wa pale waliponiona wakanichangamkia nikawambia nmeshaita gari..nafikiri hapo ndiyo wakawa wananilia mingo..ilipokuja ubber tu..wale madereva taxi wakanza kusumbua jamaa..wakawaita wale sumar JKT .ilikua sort of usumbufu.
 
Ubber mbona zipo hadi viwanja vikubwa tu vya kimataifa..tena unakuta kabisa zimeandikwa ubber
Kweli zipo lakini ujue airports zinatengeneza hela sana
Kwa mfano Heathrow airport kuna designated areas ambapo uber wakiingia hiyo parking wanalipa £4 kila wakati
Wanaacha gari hapo na kumfuata mteja na kurudi nae parking
Sasa JKN Airport lazima wajiongeze
 
Hao madereva local wana nongwa na madereva wa uber kwasababu bei zao ni fair.
 
Ilikuwa zamani siku hizi wanaingia na kufanya biashara Kama kawaida
 
Sijajua unamaanisha nini unaposema "UBA haziruhusiwi" wale madereva tax wa airport kuna chama chao na kama sikosei kuna malipo wanalipa kwa kupaki pale kwa ajili ya kusubiria abiria.

Kwa mtazamo wangu, dereva wa UBA kusubiria foleni na abiria ambae hana ahadi nae pale ni hasara vilevile itamlazimu aingie kwenye huo umoja kitu kinachoongeza gharama za kazi yake.

Naamini ukiita UBA kuja kukuchukua airport, gari itakuja na kukuchukua bila wasiwasi, ilimradi airport gari binafsi zinaruhusiwa, sioni kwanini UBA izuiliwe kuingia na kutoka maadam analipa parking. Ikumbukwe hazina utambulisho wowote wa kufanya zijulikane na kuzuiliwa kuingia uwanja wa ndege.
Kuzifahamu ni rahisi, Tax za kawaida zina Sticker Imeandikwa Airport ubavuni. Uber hazina sticker na zinakusa na plate number nyeupe
 
Kuzifahamu ni rahisi, Tax za kawaida zina Sticker Imeandikwa Airport ubavuni. Uber hazina sticker na zinakusa na plate number nyeupe

Sio zote. Kuna watu wanamagari binafsi wamesajili uba, hauwezi kuzitofautisha. Kwa ufupi ni kama tax bubu.
 
Mi nikishuka zangu natoka nje Puma pale nakula bodaboda hadi nilikopaki gari fresh,niliwahi kupaki gari mle ndani kwa wiki moja niliimba alelele…bado kuna ujinga kwamba aliepanda ndege ana hela sana,dhana potofu na ya kipumbafu
Hahahaaaa walikudindua kwa gharama nini mkuu mpaka ukaimba aleleleeee
 
Na mimi nilitaki nitoe angalizo hili hili. i.e. Ukichukua Uber eg mjini kwenda airport utapelekwa vizuri tu kwani hazina utambulisho hivyo zinaingia kama gari lolote binafsi linapompeleka msafiri. Na wakati wa kutoka vile vile ukimwita mwenye Uber anaweza kuja kama gari binafsi linapokuja na kukuchukua. Labda kama utakuwa unawazodowa wenye tax pale kuwa ''subiri niite Uber nyie si mnajifanya wajanja''!.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Dah mpwa leo nimeshindwa kabisa kukuelewa hapa, huwa najitahidi sana nikisoma text zako between the lines nakuelewa ila leo naona nimetoka kapa embu andika tena.
OK MPWA
Zile tax NI ZA WAKUBWA WENGI WA TAA
Sasa UNAPOSEMA WABEBE ABIRIA N SAWAA NA KYRUHUSUUFAMILIAAA IFE NJAAA(CHOOKILAINI)
S
Zi
 
Kuzifahamu ni rahisi, Tax za kawaida zina Sticker Imeandikwa Airport ubavuni. Uber hazina sticker na zinakusa na plate number nyeupe
Sio kila uber ina number nyeupe,zipo nyingi sana tu zenye number plates za njano,usikariri
 
Na mimi nilitaki nitoe angalizo hili hili. i.e. Ukichukua Uber eg mjini kwenda airport utapelekwa vizuri tu kwani hazina utambulisho hivyo zinaingia kama gari lolote binafsi linapompeleka msafiri. Na wakati wa kutoka vile vile ukimwita mwenye Uber anaweza kuja kama gari binafsi linapokuja na kukuchukua. Labda kama utakuwa unawazodowa wenye tax pale kuwa ''subiri niite Uber nyie si mnajifanya wajanja''!.
Nahisi unajidanganya hapa...hawa Uber wanaplate number za biashara na hivo wanafahamika vema na wenzao...pia ni kweli kuwa madreva taksi wenzao huwa hawawapendi pale airport hivo wanachokifanya hawa uber ni kumchukua abiria anaekuwa ameshuka na ndege wakti anapokuwa anaelekea airport kumpeleka abiria mwingine

Au akiwa hana abiria ataenda na gari na kuipaki eneo la parking akipata mteja atamuiya eneo hilo na kumpakia kama gari binafsi kwa tahadhari na kiondoka
 
OK MPWA
Zile tax NI ZA WAKUBWA WENGI WA TAA
Sasa UNAPOSEMA WABEBE ABIRIA N SAWAA NA KYRUHUSUUFAMILIAAA IFE NJAAA(CHOOKILAINI)
S
Zi
Haaaaa ok sawa nimekusoma mpwa, pamoja sana
 
Nani kakwmbia uber hairuhusiwi airport? Mm majuzi tu nimesubiri usafiri pale ukachelewa nikaamua kuita uber ikaja nikaondoka!
 
Back
Top Bottom