Kuna tetesi kwamba zile taxi pale airport ni za wafanyakazi wa pale pale airport.
Lakini pia, kijiwe kama kile kuna wazee wa siku nyingi ambao wanaumoja wao, Na hata wanaweza kukuroga kama ukitaka kuingia kwenye himaya yao. Hawajui sehemu nyingine zaidi ya pale.
La mwisho nadhani pia katika sehemu ambayo inaweza kuharibu taswira ya nchi kwa wageni kuibiwa ni airport. Wageni wengi wanashauriwa wachukue only registered taxi. Na kweli karibia taxi drivers wote pale airport ni waaminifu kwa sababu hapo ndipo ofisi ilipo.