Kwanini Uganda na Egypt hawana mgao wa umeme na wanategemea maji kuzalisha umeme?

Shida kubwa katika nchi hii mawaziri kuingia mikataba bila kufika kwa wananchi yaani bungeni ili kujadiliwa kujua manufaa yake. Ndio maana akiingia kiongozi fulani anaona mwenzeka kaharibu alitakiwa kufanya hivi na hii yote ni kutaka kupata tenda mpya ambayo na yeye atapata maslahi

Hii ndio inasababisha miradi kuishia njiana huku pesa imetumika bila kutoa matoke chanya
 
Ziwa victoria huku tz halipo?
 
Hata sisi Mambo ya mgao tulishayamaliza,Ila Sasa ndo tunshangaa haka kajamaa kanatulazimisha mgao.
 
Hamna swali la Kijinga Isipokuwa muulizwaji anaweza kuona la Kijinga kwasababu ya ujinga wake.
Kwani ujinga ni shida mkuu, mbona hapa umetambua jibu wewe mwenyewe na ujinga ukakutoka hapohapo kuhusu swala hilo la mafuriko yanayoweza kusababishwa Kisumu kwa matendo yanayofanyika Uganda, hata kama Kisumu yenyewe haipo Uganda?

Wakati mwingine inafaa kujiongeza tu na kuona jinsi ulivyokuwa na ujinga hapo mwanzo ulipohoji jambo ambalo hukuwa na ufahamu nalo..
Sioni ni kwa vipi anayekutoa ujinga ndiye awe mjinga, labda kama unataka tu kuendeleza mambo mengine baada ya kufundishwa kitu ambacho hukukijua.
 
Kukubali kuwa umekosea ni busara, Mkuu kubali tu kuwa Kisumu haipo Uganda Bali ipo Kenya, Hilo tu.
 
Hivi Nchi ilipofikia kuikomboa ni apatikane mtu aliye nje ya mfumo wa siasa za Tanzania aweke mifumo sawa
Huyo mtu ataingilia wapi na atatoboa vipi? Maana kama kupitia sanduku la kura hawezi kupewa chochote kinachoitwa ushindi😅!

Labda CCM yote iuawe asibakie mtu
 

Umeandika kama kokolo, childish advises, hujui unaloandika, ni story za vijiweni
 
Miongoni mwa kinachotakiwa kurekebishwa na kuwekwa sawa ni sheria za mikataba lazma iweke wazi kila mtu aweze ku access na kuusoma ama ziwekwe parameters za mikataba ya wawekezaji juu ya kile ambacho tunatakiwa kukipata kama taifa tokana na kila mkataba wa aina hio!

Kwanza muwekezaji asimiliki hio rasilimali by 100% nje ya kiwanda bali tukutane upande wa faida tu ikiwa ni 60/40kama hataki basi hamna waziri kusaini. Sio unamkabidhi mtu kitalu kinakuwa chake halafu mnaanza kulia lia anaipa serikali 5% na wizara iko kimya huku yeye anakunja 95% kumbe kuna waziri kwa baraka za raisi katengeneza 15% yake kimya kimya wanakula na raisi.

Mikataba iwe renewable and revised kila baada ya miaka 10 sio mtu anasinishwa mkataba wa milele! Ukiwa wa kipuuzi unatesa vizazi na vizazi! Kama hauna tija basi ku cancel iwepo.

Adhabu ya kunyongwa ama kupopolewa mawe hadharani na wananchi wenye hasira kali iwe kwa viongozi wote wala rushwa na mafisadi! Ikidhibitika tu mtu amefanya ucengerema iwe hakimu, speaker au raisi ni kipigo cha mbwa koko tu! Demokrasia iwepo sio kisiasa bali kwa utendaji. Bila kuwa na adhabu kali dhidi ya hawa washenzi wa CCM wataendelea kugombania madaraka na kujineemesha milele na milele huku wananchi tukipitia magumu miaka yote.
 
Kukubali kuwa umekosea ni busara, Mkuu kubali tu kuwa Kisumu haipo Uganda Bali ipo Kenya, Hilo tu.
Usitafute kunishangaza. Hivi nimeandika mahali popote kwamba Kisumu ipo Uganda, mbona unakuwa mtu usiyetaka kuelewa licha ya kukueleza kwa kurudia mara kadhaa!

Hivi jambo likifanyika Uganda, la kuzuia maji ya mto naili, tukio hilo haliwezi kusababisha mafuriko Kisumu, hata kama Kisumu haipo Uganda?

Hivi bado huelewi tu, wewe ni mtu mwenye akili za namna gani!
 
Mimi ni great thinker,unapoleta hoja hapa jukwaani lazima ujipange.
 
Mkuu 'comte', naona umetoa viambatanisho kadhaa hapa kuonyesha kwamba Egypt na wao tatizo la umeme linawakabili kama ilivyo huku kwetu.
Lakini kwao naona wananchi hawataki mchezo kabisa, hadi kuiangusha serikali. Kwa hilo wao na sisi tupo tofauti sana.

Utofauti wao na sisi pia upo kwenye kiasi cha umeme wanachozalisha na wingi wa watu wanaofaidika na umeme huo.

Egypt ni nchi mojawapo yenye umeme wa bei ya cheee barani Afrika, kiasi kwamba gharama za uzalishaji bidhaa viwandani kama simenti/clinker ni nafuu zaidi na ndio maana hata wanawauzia wenzao kwenye soko lao la COMESA bidhaa nyingi, kwa vile uzalishaji wao ni 'competitive' kulinganisha na nchi zingine kwenye umoja huo.

Kwa hiyo, nadhanipamoja na matukio hayo uliyoyaweka hapa kama ushahidi mlinganisho wa Egypt na sisi haviendani sana. Sisi tupo chini sana.

Lakini inashangaza pia kuhusu hiyo "corruption" wanayokumbana nayo. Katika hili naona wao na sisi hatuchekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…