Mimi nimeshasema nitapanda basi linaloendeshwa na mzee ikiwa ilo basi litasafiri mchana ila usiku nitamwomba apumzike ampishe kijana ambae ubongo wake bado unachemka na anauwezo wa kuhimili changamoto zote za usiki ukiwepo usingizi.
Mfano: Mwezi wa 2 mwaka huu nilipanda basi la Newforce dreva ni mzee kutokana na uchovu na usingizi nusura atuue pale rungemba mafinga sababu ya uzee wake.
Shekilango kuna abiria wawili wenzangu wakawa wananiuliza dreva mbona mzee kweli ataweza kuendesha basi usiku ? Mie nikawajibu tuombe tu Mungu atufikishe salama .
Lakini dreva alizidiwa na usingizi akaligonga roli kwa nyuma na basi likachochora polini kilichotuokoa lisipinduke ni miti mikubwa ililiziuia lisisonge mbele kwenye msitu.
Polisi walinisema sana kisa nilifunga mdomo wakisisitiza next time ukiona dreva haelewekwi fumbua mdomo wako usicheke nao hatari kwa maisha yenu abiria.