Kwanini ukitoka polisi/jela ndugu wanakwambia uvue nguo zako ili zichomwe moto

Huwa wanahisi zinakuwa na mikosi usije ukarudi tena jela Kwa makosa yaleyale ambayo umeyatumikia πŸ˜€πŸ˜„
 
Siyo tu zichomwe.
Yaani kabla hajakanyaga maeneo ya nyumbani ni lazima uoge na ubadili hizo nguo.
Zipigwe moto ndipo uelekee nyumbani ukasalimiane na nduguzo.
 
Wengi wanadai kuingia selo ni mikosi sijui pengine mikosi inaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine nazungumzia mamikosi ya watu unaokutana nao mle selo,ila kiuhalisi mle kuna majitu yenye laana na mikosi,kuna miuaji,mibakaji,na mijitu mingine ya hovyo hovyo
 
Mimi niliwai kukutana na kachero mmoja tukapishana KAULI Nika mchana aache uaskari wa kijima ule wa feudal mode of production 😊😊😊

Akanikamata kimabavu akanipiga pingu na kunisukuma nikamwelekeza P.G.O 😊😊 yule Askari alijutiaga vile vitendo tukaja suluhishwa na kushikana mikono kwa amani
Nikasikia maaskar wakiambizana Hawa vijana wa dar es salama sio wa kuendea kichwa kichwaπŸ˜…πŸ˜…

Mimi sikufuata huo muongozo Mbona na sijawai kurudi Tena kituoni kwa kosa lolote na sikuchoma nguo zangu (hiyo Ni mythology)
 
Mim
Mimi nilifunzwa hata ukitoka msibani hasa kufanya mazishi,kabla hauja beba ama kuwashika watoto wako anzia bafuni kaoge na ubadili nguo zifuliwe kivyake.

Hata sisi wenye safari ambazo njia hupita porini,ukifika nyumbani ni mhimu uoge na ubadili nguo ndipo ukaonane na watoto na hasa wale wadogo.

Sasa hawa mabinti wa Kichina ambao muda woote ni vikao vya vikoba mara sinema zao atachangamka kukuwekea maji ya kuoga kwa wakati?

Basi sisi watata unachelewa kuingia nyumbani kidogo ili kama ulipitia maporini na mkeo ni mtu wa vicoba basi ukute watoto wamelala tayari.
 
Good vijana wengi kazi ubishi tu na kujikuta wajuaji huku tukiwa hatujui kitu
 
KAZI NYINGINE HII
 
Afisa ulivyopita pita hapa kama sijakuelewa vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…