Kwanini ukitoka polisi/jela ndugu wanakwambia uvue nguo zako ili zichomwe moto

Kwanini ukitoka polisi/jela ndugu wanakwambia uvue nguo zako ili zichomwe moto

Wakuu leo hapa nyumbani nimetengewa ugali, nile tonge ngapi?
 
Nadhani mambo ya Imani zaidi .

Kwetu Bukoba huwa wanaoga dawa ukitoka nyuma ya nondo hauwezi kuingia ndani bila kuoga dawa.

Kuhusu kuchoma nguo hwazichomi Ila hauwezi kuingia ndani bila kuoga dawa.

Kuna dawa za kihaya unaoga ili uondoe mikosi.
 
Hakika inanifanya kuleta Threads mpya ya kuangazia juu ya masuala ya hizi lockup ndogo mpaka Magereza

Ukitoka nyuma ya nondo nadhani ni vyema ukajitakasa ikiwemo kufanya manuizo ya kuikataa hiyo hali.

Maana kuna watu wakiingia jela mara moja ndo yanakuwa maisha yake kila siku. Ingia toka inaanza.

So hayo mambo ni ya kiimani zaidi
 
Habari wana Jf tupeane pole juu ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Nchini.

Juzi kati nilipata msala mdogo amabao ulinipelekea kuwekwa Selo pale kituo cha polisi msimbazi.

Baada ya kusolve na kutolewa tulielekea moja kwa moja mpka home lakini ajabu baada ya kufika home.

Mzee na B mkubwa walinizuia kuingia ndani na zile nguo wakidai inatakiwa niende nikazitolee chooni kisha baada ya hapo zikachomwe moto Wazee nilistaajabu sana anyway wanaojua zaidi waje watujuze.
Iman tu
 
Mim

Mimi nilifunzwa hata ukitoka msibani hasa kufanya mazishi,kabla hauja beba ama kuwashika watoto wako anzia bafuni kaoge na ubadili nguo zifuliwe kivyake.

Hata sisi wenye safari ambazo njia hupita porini,ukifika nyumbani ni mhimu uoge na ubadili nguo ndipo ukaonane na watoto na hasa wale wadogo.

Sasa hawa mabinti wa Kichina ambao muda woote ni vikao vya vikoba mara sinema zao atachangamka kukuwekea maji ya kuoga kwa wakati?

Basi sisi watata unachelewa kuingia nyumbani kidogo ili kama ulipitia maporini na mkeo ni mtu wa vicoba basi ukute watoto wamelala tayari.
Hii ya kupita njia yenye mapori au kama ulikua una shughuli maporini niliwahi kusikia kwa mzee wa jirani yetu na yeye alisema ukitoka au kupita hizo sehemu lazima uoge na nguo zikafuliwe ndo uje ujumuike na wengine hasa watoto na alisema hutakiwi kuingia chooni au kuoga bafu lenye choo ndani,, ukishaoga na kubadili nguo ndo unaweza kuingia chooni
 
Ni imani tu, kwani mpaka unaenda selo nguo hizo zishawahi kwenda selo, jibu hapana, so ni imani tu, ila kwa heshima ya wazee unatii tu, huku moyoni ukijua hakuna lolote.
 
Hii ya kupita njia yenye mapori au kama ulikua una shughuli maporini niliwahi kusikia kwa mzee wa jirani yetu na yeye alisema ukitoka au kupita hizo sehemu lazima uoge na nguo zikafuliwe ndo uje ujumuike na wengine hasa watoto na alisema hutakiwi kuingia chooni au kuoga bafu lenye choo ndani,, ukishaoga na kubadili nguo ndo unaweza kuingia chooni
Hii ni kwa7bu huenda huko porini tupitako kukawa kumetupwa mizoga au mwili wa binadamu aliyeuawa ama kajiua na pengine hata bila kuiona.
 
Habari wana Jf tupeane pole juu ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Nchini.

Juzi kati nilipata msala mdogo amabao ulinipelekea kuwekwa Selo pale kituo cha polisi msimbazi.

Baada ya kusolve na kutolewa tulielekea moja kwa moja mpka home lakini ajabu baada ya kufika home.

Mzee na B mkubwa walinizuia kuingia ndani na zile nguo wakidai inatakiwa niende nikazitolee chooni kisha baada ya hapo zikachomwe moto Wazee nilistaajabu sana anyway wanaojua zaidi waje watujuze.
Je ulichoma Saa na Wallet.....?
 
Back
Top Bottom