Kwanini ukitoka polisi/jela ndugu wanakwambia uvue nguo zako ili zichomwe moto

Wakuu leo hapa nyumbani nimetengewa ugali, nile tonge ngapi?
 
Nadhani mambo ya Imani zaidi .

Kwetu Bukoba huwa wanaoga dawa ukitoka nyuma ya nondo hauwezi kuingia ndani bila kuoga dawa.

Kuhusu kuchoma nguo hwazichomi Ila hauwezi kuingia ndani bila kuoga dawa.

Kuna dawa za kihaya unaoga ili uondoe mikosi.
 
Hakika inanifanya kuleta Threads mpya ya kuangazia juu ya masuala ya hizi lockup ndogo mpaka Magereza


Ukitoka nyuma ya nondo nadhani ni vyema ukajitakasa ikiwemo kufanya manuizo ya kuikataa hiyo hali.

Maana kuna watu wakiingia jela mara moja ndo yanakuwa maisha yake kila siku. Ingia toka inaanza.

So hayo mambo ni ya kiimani zaidi
 
Iman tu
 
Hii ya kupita njia yenye mapori au kama ulikua una shughuli maporini niliwahi kusikia kwa mzee wa jirani yetu na yeye alisema ukitoka au kupita hizo sehemu lazima uoge na nguo zikafuliwe ndo uje ujumuike na wengine hasa watoto na alisema hutakiwi kuingia chooni au kuoga bafu lenye choo ndani,, ukishaoga na kubadili nguo ndo unaweza kuingia chooni
 
Ni imani tu, kwani mpaka unaenda selo nguo hizo zishawahi kwenda selo, jibu hapana, so ni imani tu, ila kwa heshima ya wazee unatii tu, huku moyoni ukijua hakuna lolote.
 
Hii ni kwa7bu huenda huko porini tupitako kukawa kumetupwa mizoga au mwili wa binadamu aliyeuawa ama kajiua na pengine hata bila kuiona.
 
Je ulichoma Saa na Wallet.....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…