Kwanini ukiwafanya wadada wa kazi kama ndugu hawadumu, ila ukiwaendesha kama chuma cha Mjerumani utakaa nao miaka?

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
​

Nadhani wengi tuna experience kwenye hili. Yaani ukimtendea vizuri dada wa kazi na kumfanya kama mwanafamilia au kama mtoto wako lazima uishie kujuta! Utapigwa matukio hadi mwenyewe unyooshe mikono, atakaa miezi kadhaa tu utasikia mimi nataka kuondoka, sijui nimemiss kwetu, mara nyingine unashtukia hayupo, huyoo katoroka zake.

Sasa, pigisha kazi kama chuma ya Mjerumani, aloo anaweza kukaa hata miaka kumi na kila kitu kinaenda shwari kabisa! Kuna sayansi gani hapa? Ndo wote wameshazoea mikiki mikiki ama?

Tulikuwa na huyo ndugu yetu, yeye binti wa kazi akiondoka kwake anakuwa amekaa si chini ya miaka mitano. Lakini kwa namna anavyowatendea utaona huruma, kwanza familia kubwa (watu 7) na kuna watoto wa kuhudumia, kuamka mapemaaa kulala usiku mwingi, dada analia jikoni huko peke yake, marufuku kufika sebuleni labda awe analeta chakula au anasafisha, muda wote ye yuko na shughuli, mpaka aje kulala yuko hoi.

Sasa njoo kwa mwenzangu na mimi jifanye unamuona kama mdogo wako, ataamka muda anaotaka, muda mwingi yupo kwenye simu mara TV, unakuta vitu rafu mpaka wewe ndio unakuwa kama umeajiriwa sasa na yeye ndio Boss wako.

Kwanini iko hivi eti?🤔🤔
 
siyo kweli, unatakiwa tu uwe fair, afanye kazi na alipwe stahiki zake kulingana na kazi anazofanya, ni binadamu pia hivyo anashahili kupumzika na hata likizo kuwasalimia ndugu na jamaa zake, kuwa na boyfriend (akipata mtu siyo shida yako na usimuingilie wala kumpangia), last but not least mlipe ujira wake, hayo mengine yote hayahitajiki ...
 
Wasichana wa kazi hawakai.
 
Sisi Kuna mmoja alikuja siku ya tatu akasema anataka kuondoka! Hapo nimemtoa mkoani! Mwingine kakaa mwezi, yaani hata hatujamzoea vizuri. Mwaka fulani tukapata msichana anajua sana kazi, kuamka saa 11 mwenyewe bila kuamshwa saa tatu kamaliza kazi zote (kufua nguo za watoto, kudeki na kufagia na chai, uji. Huyo alikaa mwaka mzima. Tukasema tumwongezee mshahara ili aendelee kudumu. Mshahara ukapanda kutoka 80k mpaka 150. Cha ajabu baada ya mshahara kupanda mwezi wa pili tu akaomba kuondoka! Baada ya hapo ni leta ondoka! Mwishowe tukaachana nao. Mwaka wa 4 hatuna msichana.
 
kumbe ndivyo mlivyo na roho mbaya namna hiyo ninyi wamama?

huenda ndio maana wadada wengine hua makatili zaidi kwa watoto wa familia na saa zingine kuwaangamiza kabisa. Kumbe huwa wanafanya hivyo kama kisasi cha hila za makusudi mnazowatendea?

Badilikeni tafadhali wamama plz plz, roho mbaya haijengi inabomoa tu 🐒
 
Nimeona hili wanalizungumzia mahali imekaaje?

Expiriensi ya kwangu kutoka nyumbani kwetu tumekaa na wadada wa kazi up to 7 years, kama Walikuwa wanakaa vizuri au vibaya i can’t judge, ila literally they were like mamdogo to us, Maana mama yetu mtafutaji kila kitu walikuwa wanafanya wao.

Walikuwa wanakuwa wawili wawili mmoja anaweza kukaa 3 years mwingine 4 na zaidi.
 
Mfanyakazi mpe stahiki usimtese, mpe uhuru mpe siku moja ya mapumziko nae aende akafanye yake!.
akikosea kama una weza piga huwezi mseme asiyajue sana yako hapo mtaishi
Mimi Mke wangu anachukua Ndugu zake wale wa vijijini ambao wangebaki huko wangebebeshwa Mimba Tu na maisha yao magumu, wakishajua Mjini wanakula Chakula kizuri kwa BushDokta, wanalala pazuri na lotion nzuri nzuri aisee nimeshaozesha watatu.

Kwenye hili Mungu ni Mwema
 
Mi sihitaji stress za kukaa na ndugu.
Wangu nimeishi nae miaka 18 nahitaji kumfukuza sioni jinsi ya kuanza kumfukuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…