Kwanini ukiwafanya wadada wa kazi kama ndugu hawadumu, ila ukiwaendesha kama chuma cha Mjerumani utakaa nao miaka?

Kwanini ukiwafanya wadada wa kazi kama ndugu hawadumu, ila ukiwaendesha kama chuma cha Mjerumani utakaa nao miaka?

Mtuache wababa tukae nao hata mwezi

Sasa post niliyokutana nayo juzi ni mbaba ndo alikuwa analalamika! Yeye ni single father, anasema ndani ya mwaka kashabadili wadada kama 6! Alipatapata cha moto😂😂 yaani haijalishi Boss ni nani, ila ukimfanya kama mwanafamilia tu inakula kwako!
 
Huyu dada zamani nilikuwa namtandika tena nilishamtandika sana baada ya kutoroka na kuwekwa geto na kuambulia mimba.
Pia lazima nitandike mtu anayelta masela kwangu na wanachezea wifi na kudinyana kwangu.

Lakini toka apigwe mimba na kuachwa akili iko sawa hata nikisafiri mwaka mzima anabaki yeye na mbwa tu hakuna anaye ingia ndani
😂😂😂
 
Anaondoka ukimfanya kama familia kwa sababu anakua ameshapata mtaji wa kujitegemea baada ya kukuibia

Ulivyomaliza hapo mwishoni😂😂 inawezekana ila itakuwa % ndogo, maana wengi huishia kutangatanga tu na sio kwenda kusimama mwenyewe
 
Kazi za ndani hazipaswi kuwa ajira ya mtu ya kudumu, inapaswa kuwa kwa ajili ya kupita tu kuelekea maisha mengine mazuri zaidi.

Hilo ni kweli, lkn ndio mtu adumu kwa mwezi moja, miwili, mitatu?
 
Sisi Kuna mmoja alikuja siku ya tatu akasema anataka kuondoka! Hapo nimemtoa mkoani! Mwingine kakaa mwezi, yaani hata hatujamzoea vizuri. Mwaka fulani tukapata msichana anajua sana kazi, kuamka saa 11 mwenyewe bila kuamshwa saa tatu kamaliza kazi zote (kufua nguo za watoto, kudeki na kufagia na chai, uji. Huyo alikaa mwaka mzima. Tukasema tumwongezee mshahara ili aendelee kudumu. Mshahara ukapanda kutoka 80k mpaka 150. Cha ajabu baada ya mshahara kupanda mwezi wa pili tu akaomba kuondoka! Baada ya hapo ni leta ondoka! Mwishowe tukaachana nao. Mwaka wa 4 hatuna msichana.

Yaani sijui huwa nini kinatokea!
 
kumbe ndivyo mlivyo na roho mbaya namna hiyo ninyi wamama?

huenda ndio maana wadada wengine hua makatili zaidi kwa watoto wa familia na saa zingine kuwaangamiza kabisa. Kumbe huwa wanafanya hivyo kama kisasi cha hila za makusudi mnazowatendea?

Badilikeni tafadhali wamama plz plz, roho mbaya haijengi inabomoa tu 🐒

Ukisharudisha ubongo kichwani urudi sasa kuchangia mada Mkuu!
 
Nimeona hili wanalizungumzia mahali imekaaje?

Expiriensi ya kwangu kutoka nyumbani kwetu tumekaa na wadada wa kazi up to 7 years, kama Walikuwa wanakaa vizuri au vibaya i can’t judge, ila literally they were like mamdogo to us, Maana mama yetu mtafutaji kila kitu walikuwa wanafanya wao.

Walikuwa wanakuwa wawili wawili mmoja anaweza kukaa 3 years mwingine 4 na zaidi.

Tuliwahi bahatisha mmoja pia tukiwa wadogo, she practically raised us! Nadhani tulikaa nae karibu miaka 10, baada ya hapo ni majanga tu, tulikujaga bahatisha mwingine mmoja baada ya muda mrefu kupita mpaka akapata mchumba na kuolewa
 
Ulivyomaliza hapo mwishoni😂😂 inawezekana ila itakuwa % ndogo, maana wengi huishia kutangatanga tu na sio kwenda kusimama mwenyewe
Chunguza kwa wanaowafanya kama familia, kuiba na kuweza kujitegemea ni kitu kingine
 
Ingependeza kuwaajili watu wazima yaani wamama ili kipato chao wakalipie ada za watoto wao,na sio lazima walale hapo waje na kuondoka,wadada hamuwaonei huruma?? They too need to have their future, kuwafungia ndani na malipo ya lakimoja au alfu 50 mhhhh vinginevo kama mtakuwa mnawasomesha.

Umeelewa mada kweli ndugu?🤔🤔
 
Kuna muda sisi waafrica bila kutumia nguvu hatuelewi!!
Alikuwa ananidharau baada ya kumkata mitama ni miaka sasa heshima imetawala

Kaaaah! Kumbe ulimaanisha kumpiga - kumchapa, unafaa kuchukuliwa hatua za kisheria wewe
 
Back
Top Bottom