Kwanini ukiwafanya wadada wa kazi kama ndugu hawadumu, ila ukiwaendesha kama chuma cha Mjerumani utakaa nao miaka?

Kwanini ukiwafanya wadada wa kazi kama ndugu hawadumu, ila ukiwaendesha kama chuma cha Mjerumani utakaa nao miaka?


Nadhani wengi tuna experience kwenye hili. Yaani ukimtendea vizuri dada wa kazi na kumfanya kama mwanafamilia au kama mtoto wako lazima uishie kujuta! Utapigwa matukio hadi mwenyewe unyooshe mikono, atakaa miezi kadhaa tu utasikia mimi nataka kuondoka, sijui nimemiss kwetu, mara nyingine unashtukia hayupo, huyoo katoroka zake.

Sasa, pigisha kazi kama chuma ya Mjerumani, aloo anaweza kukaa hata miaka kumi na kila kitu kinaenda shwari kabisa! Kuna sayansi gani hapa? Ndo wote wameshazoea mikiki mikiki ama?

Tulikuwa na huyo ndugu yetu, yeye binti wa kazi akiondoka kwake anakuwa amekaa si chini ya miaka mitano. Lakini kwa namna anavyowatendea utaona huruma, kwanza familia kubwa (watu 7) na kuna watoto wa kuhudumia, kuamka mapemaaa kulala usiku mwingi, dada analia jikoni huko peke yake, marufuku kufika sebuleni labda awe analeta chakula au anasafisha, muda wote ye yuko na shughuli, mpaka aje kulala yuko hoi.

Sasa njoo kwa mwenzangu na mimi jifanye unamuona kama mdogo wako, ataamka muda anaotaka, muda mwingi yupo kwenye simu mara TV, unakuta vitu rafu mpaka wewe ndio unakuwa kama umeajiriwa sasa na yeye ndio Boss wako.

Kwanini iko hivi eti?🤔🤔
Ingependeza kuwaajili watu wazima yaani wamama ili kipato chao wakalipie ada za watoto wao,na sio lazima walale hapo waje na kuondoka,wadada hamuwaonei huruma?? They too need to have their future, kuwafungia ndani na malipo ya lakimoja au alfu 50 mhhhh vinginevo kama mtakuwa mnawasomesha.
 
Mi sihitaji stress za kukaa na ndugu.
Wangu nimeishi nae miaka 18 nahitaji kumfukuza sioni jinsi ya kuanza kumfukuza
The basis, is huo mshahara unaomlipa, badala uwalipe watu baki huko vijijini kuna Ndugu ambao na wao ungewafaa na kuwasaidia.

Huyo wa kwako 18yrs bado anfanya nini
 
mmh dada kumpga tena?
Huoni hapo kumpga atalipiza kwa wanao, ukiwa haupo?
Huyu dada zamani nilikuwa namtandika tena nilishamtandika sana baada ya kutoroka na kuwekwa geto na kuambulia mimba.
Pia lazima nitandike mtu anayelta masela kwangu na wanachezea wifi na kudinyana kwangu.

Lakini toka apigwe mimba na kuachwa akili iko sawa hata nikisafiri mwaka mzima anabaki yeye na mbwa tu hakuna anaye ingia ndani
 
Huyu dada zamani nilikuwa namtandika tena nilishamtandika sana baada ya kutoroka na kuwekwa geto na kuambulia mimba.
Pia lazima nitandike mtu anayelta masela kwangu na wanachezea wifi na kudinyana kwangu.

Lakini toka apigwe mimba na kuachwa akili iko sawa hata nikisafiri mwaka mzima anabaki yeye na mbwa tu hakuna anaye ingia ndani
Yupo kwako na mtoto wake?
 
The basis, is huo mshahara unaomlipa, badala uwalipe watu baki huko vijijini kuna Ndugu ambao na wao ungewafaa na kuwasaidia.

Huyo wa kwako 18yrs bado anfanya nini
Sikuzaliwa kwa ajili ya kukomboa kijiji changu.
Ndugu nasaidia kadri ninavyojaaliwa, madhara ya kukaa na ndugu niliyaona kwa wazazi wangu hivyo kwangu niliapa sihitaji.

Anasomesha mtoto, pia mimi kwangu mimi anamaliza kazi saa 6 hivyo nilimsaidia kupata kazi fulani hivi..... pia anasema amalizie kujenga kibanda chake
 
Nimeona hili wanalizungumzia mahali imekaaje?

Expiriensi ya kwangu kutoka nyumbani kwetu tumekaa na wadada wa kazi up to 7 years, kama Walikuwa wanakaa vizuri au vibaya i can’t judge, ila literally they were like mamdogo to us, Maana mama yetu mtafutaji kila kitu walikuwa wanafanya wao.

Walikuwa wanakuwa wawili wawili mmoja anaweza kukaa 3 years mwingine 4 na zaidi.

Hao walikua zamani, tunazungumzia madada wanao lea wstoto wako.

Na sio wadada wa kazi tu, Hata job market lipo so dynamic sana.

Mm nimemaliza chuo 2022, nishafanya kazi kampuni 3 before entering government this yr.

Kwahyo watu wajipande, Sisi Gen Z tuna alternative nyingi za kuishi/kupata kipato + A lot of information ambazo sometimes zinatuchanganya.
 
SIO KWELI

MTHAMINI MTOTO WA KAZI KAMA WA KWAKO

NADHARIA ZA KUTETEA UKATILI

LOVE TRUMPS HATE
 
Sisi Kuna mmoja alikuja siku ya tatu akasema anataka kuondoka! Hapo nimemtoa mkoani! Mwingine kakaa mwezi, yaani hata hatujamzoea vizuri. Mwaka fulani tukapata msichana anajua sana kazi, kuamka saa 11 mwenyewe bila kuamshwa saa tatu kamaliza kazi zote (kufua nguo za watoto, kudeki na kufagia na chai, uji. Huyo alikaa mwaka mzima. Tukasema tumwongezee mshahara ili aendelee kudumu. Mshahara ukapanda kutoka 80k mpaka 150. Cha ajabu baada ya mshahara kupanda mwezi wa pili tu akaomba kuondoka! Baada ya hapo ni leta ondoka! Mwishowe tukaachana nao. Mwaka wa 4 hatuna msichana.
Mmejaribu mvulana? Wako hao wanafanya kazi na wanadumu.
 
siyo kweli, unatakiwa tu uwe fair, afanye kazi na alipwe stahiki zake kulingana na kazi anazofanya, ni binadamu pia hivyo anashahili kupumzika na hata likizo kuwasalimia ndugu na jamaa zake, kuwa na boyfriend (akipata mtu siyo shida yako na usimuingilie wala kumpangia), last but not least mlipe ujira wake, hayo mengine yote hayahitajiki ...

Baada ya utangulizi huo, turudi kwenye mada Mkuu!
 
Back
Top Bottom