Kwanini ukoo wako ni masikini?

Kwanini ukoo wako ni masikini?

Unmaskini unarithishwa?

Unaweza kukomaa bila mafanikio kumbe kuna madesa ya jadi uliyoaminishwa kimyakimya (subliminally) yanakuvuta shati.

Mfano, moja ya ukoo nilioufuatilia

1: Ukiwa tajiri utalogwa hadi uwe kama wenzako

2: Waliofanikiwa kidogo wanastrago kuhakikisha kila mwana ukoo anawategemea wao tu.

3: Baba, Mama, Ukoo mzima unajuhudi kubwa katika kulaani na sio kubariki, kukuza mabaya badala ya mema.

Ukiona ukoo au familia ina hizi mentality piga chini kwa hekima lakini. Ikiwezekana kaa mbali hizo ni tabia za kimasikini. Hama hata mkoa ukaanzishe ukoo na familia mpya maana utaambukizwa.
 
Kheri uwe broken, kuliko kuwa litajiri la majini yaan una ishi a ndoa ya majini...kuna chalii mmoja yupo Korogwe dogo ana hela ila kila mwezi kunantarehe ikifika dogo anajinyea .(involuntary)

Kuna dogo mwengine yupo kibaha picha ya ndege ..dogo na yy ana mpunga kajenga vijumba vya kupangisha lkn vina masharti kama kambi ya jeshi..mm huwa naviita bijumba vyake kambi ya majini..ktk bijumba ivyo mkristo hupangi nyumbaa wala frame zake, kula kiti moto marufuku, kuuza bia ktk frame zake ni marufuku..

Sasa kwa scenario izo chache hapo ivi huo utajiri utaufurahia kweli ?
Uo sio utajiri ni ujinga na utumwa.

Mungu anataka tuwe matajiri Kwa kufuata formula sio mihemko ya kiganga. Pia umaskini ni laana sio kitu cha kujivunia
 
Kaukoo ketu nikaajabu sanaa,mwenye nazo wachacheee wanataka muwasujudie...usipo jipendekeza hawakupi ramani wala msaada,ukijiweka mbalii Ni majungu na lawama oooh mtoto wa Fulani anajiskia....Mara anajitenga na wezake,michango hatoi dah hizi Koo nyingine basi ingekiwa naweza ningehamaa ukoo.....laana na kulaaniana ndo usisemeee,kulogana Nako....
Kaukoo ketu ni kaajabu mnoo. Yaan wao hawajui kutamkia watoto wao baraka. Ni laana kwa laana.
 
Hata nchi yetu kuendelea kuiita masikini ni kuarika laana Kwa vizazi vyetu.

Tunatakiwa tuiite nchi yenye rasilimali ambazo bado hazijatumika kutunufaisha, ikiwemo rasilimali ubongo
 
Ndugu ni wengi sana. Na shida zao haziishi. Na wana wivu sana. Na wanataka uwape msaada hadi ulingane nao. YANI DUNIA YA LEO UKITAKA KUFELI, Kuwa karibu na ndugu kama umefanikiwa. Najua mifano kibao watu waliajiri ndg kwa biashara nzuri zikafa kabisa.

Mimi nilishaacha kusaidia ndugu. Na nilivyoacha ndio mambo yangu yamekuwa yananyooka kweli kweli. Kwanza kufanikiwa nimepambana mwenyewe tu na Mungu wangu. Wao kwani nani aliwazuia wasipambane kama mimi? Yani mimi afadhali nisaidie mjane au mtu mgeni kuliko ndugu. Hao wasio ndugu wana shukrani sana. Ila ndg wanaona ni wajibu wako.
nimekuelewa ndugu, ila usiache kuwasiadia ndugu wenye uhitaji...

siku ukipata shida, dunia yote itakutenga ila ndugu anaweza kukukumbuka.
 
Unategemea nini mtu anafikisha miaka 40 hana ujuzi wowote achana na elimu ya darasani.
Yaani ujuzi hata wa kupika maandazi au kusuka mkeka hana.
Vicious cycle ndio inayoua ichumi wa mwafrika.
Katika familia zeti za kiswahili hatuko serious na maisha.
Din nazo zimefubaza ubongo wa mtanzania vibaya sana wala haiitaji Phd, watu wanategemea kutoboa kwa mafuta ya upako, kuomba,kuombewa, dini zingine zinatufundisha kuwa tuache tamaa ya dunia kwa sababu vyote tutaviacha huko akhera thawabu ndio mtaji hivyo basi kuna kundi la watu lipo busy kujaza thawabu kwenye vitabu vyao.
 
Unmaskini unarithishwa?

Unaweza kukomaa bila mafanikio kumbe kuna madesa ya jadi uliyoaminishwa kimyakimya (subliminally) yanakuvuta shati.

Mfano, moja ya ukoo nilioufuatilia

1: Ukiwa tajiri utalogwa hadi uwe kama wenzako

2: Waliofanikiwa kidogo wanastrago kuhakikisha kila mwana ukoo anawategemea wao tu.

3: Baba, Mama, Ukoo mzima unajuhudi kubwa katika kulaani na sio kubariki, kukuza mabaya badala ya mema.

Ukiona ukoo au familia ina hizi mentality piga chini kwa hekima lakini. Ikiwezekana kaa mbali hizo ni tabia za kimasikini. Hama hata mkoa ukaanzishe ukoo na familia mpya maana utaambukizwa.

umaskini unasababishwa na hivi
*kutokubali mabadiliko
*uliokuwepo nao mfano marafiki,kazi,biashara na elimu

hivi vitu kama utanielewa subiri kufirisika
 
Unmaskini unarithishwa?

Unaweza kukomaa bila mafanikio kumbe kuna madesa ya jadi uliyoaminishwa kimyakimya (subliminally) yanakuvuta shati.

Mfano, moja ya ukoo nilioufuatilia

1: Ukiwa tajiri utalogwa hadi uwe kama wenzako

2: Waliofanikiwa kidogo wanastrago kuhakikisha kila mwana ukoo anawategemea wao tu.

3: Baba, Mama, Ukoo mzima unajuhudi kubwa katika kulaani na sio kubariki, kukuza mabaya badala ya mema.

Ukiona ukoo au familia ina hizi mentality piga chini kwa hekima lakini. Ikiwezekana kaa mbali hizo ni tabia za kimasikini. Hama hata mkoa ukaanzishe ukoo na familia mpya maana utaambukizwa.
Fact
 
Mkuu acha kuaminisha kua wote walio masikini wana mapungufu. Mali na Fedha ni Mali ya Bwana hivyo hutoa kwa awapendao. Umaskini na utajiri umekuepo toka enzi na enzi na hautaisha. Hivyo utajiri kwako kwa mwingine ni Umaskini. Okay.... naona bandiko lako limekaa ki kufitinisha fitinisha.
Na pia ukiwa tajiri then what? Na ukiwa masikini then what? Yote ni kujilisha upepo tu
N.b. Umaskini sio Mzuri.
 
Back
Top Bottom